Chama
cha demokrasia na maendeleo {CHADEMA} kimesema Bunge maalumu la katiba
na vikao vyake vinavyoendelea hivi sasa havina uhalali wa kukubalika kwa
sababu hakuna maridhiano wala muafaka wa kitaifa hivyo limepoteza
uhalali wake kwa sababu ya kuvunjwa kwa sheria ambapo pia chama hiki
kimemtuhumu Mwenyekiti Samweli Sitta kuwa analiongoza bunge hilo kuvunja
sheria.
Aliyeyazungumza haya ni naibu katibu mkuu wa Chadema John Mnyika
ambae pia ni mbunge wa Ubungo na kuongeza kwamba kilichofanywa juzi na
bunge ni kitendo kisichovumilika kwa kuvunja sheria maalumu ya bunge kwa
kuruhusu upigwaji wa kura kwa mtu akiwa nje ya bunge.
Kabla ya kumsikiliza kwa mapana hapa chini, nataka nikupe baadhi ya
mistari iliyoandikwa na baadhi ya Magazeti ya Tanzania September 23 2014
>>>> #MWANANCHI – Bunge kutuma Ofisa Saudi Arabia kusimamia kura #TanzaniaDAIMA – UKAWA waokoa shilingi bilioni 2.3, ni kutokana na kususia bunge, katibu akiri hazijaombwa Serikalini.
No comments:
Post a Comment