Oscar
Pistorius ni mwanariadha wa Afrika Kusini ambae amekua kwenye headlines
kutokana na ishu yake ya kutuhumiwa kumuua mpenzi wake kwa risasi
Valentine’s day mwaka jana.
Taarifa
mpya za Mahakama leo zinasema Jaji ametoa maamuzi kwenye shitaka la
kwamba alifanya mauaji ya kukusudia kwamba upande wa mashtaka umeshindwa
kuthibitisha kuwa aliua kwa makusudi.
Kwenye
kesi hii Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake lakini ni kwa bahati
mbaya na sio makusudi ambapo Mwandishi wa BBC ameripoti kwamba huenda
Jaji akachukua mpaka Ijumaa kukamilisha maamuzi yake.
Ikitokea Pistorius akapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake basi anaweza kufungwa jela miaka 25.
No comments:
Post a Comment