Ulaji
wa matango na matikiti maji husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo
huitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa
cha maji ambayo husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali
ambazo miili yetu huzipata kupitia vyakula, madawa na hata vinywaji.
(1)Husaidia kupunguza uzito wa mwili. Kutokana na kuwa na asili ya nyuzi
nyuzi au, fibres, humfanya mlaji ajisikie kushiba bila ya kuongeza vitu
mwilini ambavyo husababisha mtu aongezeke uzito hivyo kuzuia magonjwa
mbalimbali
(2)Hupunguza (hangovers),uchovu, mawengewenge pamoja na hali ya
kujisikia vibaya kutokana na unywaji wa kilevi. Hii ni kutokana na kuwa
na vitamini B na maji mengi ambapo, baada ya mtu kunywa kilevi na kisha
akaja kula matango kabla ya kulala, itamfanya asubuhi asiamke huku akiwa
na hangovers
(3)Husaidia katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya tumbo kama vile
kuvimbiwa, tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo na mengineyo hupungua
kutokana na ulaji wa matango, husaidia kuondoa sumu tumboni na
kurahisisha ufyonzwaji wa protein mwilini kutokana na uwepo wa
kiwezeshaji cha kibaiolojia kinachoitwa, erepsin enzyme.
(4)Husaidia kuondoa msongo wa mawazo kwani yana kiwango kikubwa cha
vitamini B ambayo husaidia kuboresha utendaji kazi wa mishipa mbalimbali
ya fahamu mwilini na hivyo kuondoa hatari ya mtu kuathirika na msongo
wa mawazo unaosababishwa na maisha ya kila siku.
(5)Husaidia
kuondoa hatari ya mtu kupata kansa. Yana kiwango kikubwa cha
virutubisho vyenye asili ya mimea viitwavyo, lignans, ambavyo pamoja na
vitamini c,
(6)husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuiboresha kinga ya mwili na hivyo kuepusha hatari ya mtu kupata kansa.
(7)Husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani. Kwa kukiweka kipande cha
tango mdomoni kwa dakika kadhaa, huuwa bakteria mbalimbali wasababishao
magonjwa mbalimbali ya kinywa na harufu mbaya mdomoni.
(8)Husaidia mtu kupata choo laini na huzuia kukosa choo.
(9)Huzuia kuganda kwa mafuta katika mishipa ya damu ili kuwezesha
mzunguko sahihi wa damu kaitika pande zote za mwili sambamba na
kurekebisha mapigo ya moyo
(10)Huwepo wa vitamini katika matunda haya husaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini na presha.
No comments:
Post a Comment