Wakati
Serikali ikitafuta mwarobaini wa vifo vya mama na mtoto wanapojifungua,
imegundulika kuwa kuna idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda wake
(njiti), ambao hufariki dunia kila siku katika hospitali mbalimbali nchini
kutokana na ukosefu wa huduma ‘muhimu’ katika vituo vya afya.
Taarifa za kuaminika
zilizotufikia katika chumba cha habari kutoka kwa mmoja wa madaktari, ambaye
hakutaka jina lake litajwe mtandaoni, Mei 2, mwaka huu, amesema hospitali za serikali
jijini Dar es Salaam na mikoani, baadhi ya watoto hao hupoteza maisha kutokana
na kukosekana kwa mashine maalumu za kuwahifadhia zijulikanazo kama
‘Incubator’.
Kwa mujibu wa takwimu mbalimbali kuhusu tatizo hilo zinaonyesha
kuwa, zaidi ya asilimia 75 ya watoto wanaozaliwa kabla ya mda wake ‘njiti’ nchini
Tanzania, wangeweza kuokolewa pasipo kuhitaji uangalizi wa kiutaalam zaidi kama
vifaa vinavyohitajika vingekuwepo.
Hata
hivyo, katika taarifa iliyowahi kutolewa kwa ajili ya siku ya watoto Njiti
Ulimwenguni ijulikanayo kwa jina la (Kuzaliwa Mapema Mno) mwaka 2013, inakadiria
kuwa watoto 210,000 nchini Tanzania wanazaliwa kabla ya muda kila mwaka
kutokana na tatizo hilo.
Zaidi
ya theluthi moja ya vifo vya watoto wanaokadiriwa kufikia 40,000 nchini
Tanzania, hufa kila mwaka kutokana na matatizo ya kuzaliwa kabla ya kutimiza
muda, ambapo mtoto anatakiwa kuzaliwa kwa kawaida akiwa na uzito wa karibu kilo
tatu (2.8Kg) kwa wastani na urefu wa sentimeta hamsini, mimba ikiwa imefikia
wiki ya 38 hadi 42.
Aidha,
Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zimethibitishwa kuwa
zimefikia lengo la maendeleo ya Milenia namba 4 juu ya uhai wa mtoto, huku matatizo
ya watoto kuzaliwa kabla ya muda yakiwa yanashika nafasi ya pili katika
kusababisha vifo vya watoto, baada ya homa ya kifua.
Takwimuya
Shirika la Afya duniani (WHO) inaonyesha kuwa asilimia 17 ya watoto
wachangakatika nchi zinazoendelea wanakabiliwa na uzito pungufu wa
kuzaliwa, ikilinganishwana asilimia 13 ya watoto wanaozaliwa nchini
Tanzania.
No comments:
Post a Comment