TANZANIA
inatajwa kuwa miongozi mwa Nchi zinazoendelea, kuwa na Idadi kubwa ya
Watu wanaosumbuliwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ambapo zaidi ya
Watu (milioni Nane) hufariki kila mwaka kutokana na Magonjwa hayo.
Takwimu
za Kidunia pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) za mwaka 2012/2013,
zinaonyesha kuwa karibu Watu milioni 35 hufariki ndani ya mwaka mmoja,
hali ambayo inachangaia kushuka kwa Uchumi.
Katika
mpangowa upimaji wa Afya kwa magonjwa yasiyoambukiza Jijini Dar es
salaam, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umebaini kuwa Idadi kubwa
ya Wanaume wanapatwa na magonjwa hayo kuliko Wanawake.
Uchambuzi
huo umeonyesha magonjwa yasiyoambukiza Kama, Kisukari, Shinikizo la
damu, na Saratani zote ambazo zimekuwa chanzo cha Vifo hivyo, huku
Serikali ikisema imeamua kuongeza juhudi za makusudi kupambana nayo.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Mfuko wa bima ya Afya, athari ya magonjwa
yasiyoambukiza ni mara (Nne) zaidi ya watu waliopo mijini kuliko
vijijini, huku asilimia 12.8 ya wanaougua wakiwa wako mijini na aslimia
3.1 wako vijijini kutokana na mfumo wa maisha.
No comments:
Post a Comment