Kazi ilipokamilika nyumbani kwao
alipoitengenezea, Polisi wa mji huo wakamkataza kuipaisha kwa sababu ni
kinyume na sheria lakini ili kuepuka kumkatisha tamaa… wakamwambia ni
vyema akapata kibali kutoka kwa mamlaka ya anga.
Paul Karanja alizuiwa na polisi
kuipaisha hii ndege kutoka uwanja wa mdogo wa ndege wa Karagita na
kuwanyima uhondo zaidi ya watu 500 waliofika asubuhi ya saa 3 kuangalia
chombo kikipaishwa.
Hata hivyo
Mwanachuo huyu wa chuo kikuu cha Meru ana imani ataipaisha ndege yake
siku moja ili kutimiza ndoto yake ambayo hata hivyo ilipata hitilafu
kwenye uwanja wa ndege wa Karagita kutokana na hali mbaya ya uwanja huu
iliyosababisha tairi la ndege yake kuharibika.
Karanja ambae ni Mwalimu pia wa shule
ya upili, amesema tayari ameiandikia barua mamlaka ya ndege nchini Kenya
kuhusu kupaisha ndege hiyo lakini hajapata majibu.(awadh ibrahim)
No comments:
Post a Comment