Kenny Mwangoka akiendesha gari hilo ambalo bodi lake limetengenezwa kwa mbao |
Kenny Mwangoka akifungua mlango wa nyuma wa gari hilo akionesha ubora na umaridadi wa lake |
Mwanahabari huyu Oliva Motto wa Star TV hakuamini kama kilichounda bodi ya gari hilo ni mbao mpaka alipogusa na kujiridhisha |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Peter Tweve akistaajabu kwa mshangao mkubwa ubunifu aliouonesha Mwangoka na kuamua kumpongeza kwa ubinifu huo |
Gari hili linamilikiwa na mvunaji na mfanyabishara wa mbao wa Nyololo, Mafinga, Kenny Mwangoka.
Mwangoka alilinunua gari hilo lililokuwa linamilikiwa na mission ya kanisa katoliki Mafinga baada ya kupata ajali na kuharibika vibaya.
Jitihada za Mwangoka kulifufua gari hilo kwa kuvisha bodi mpya hazikuzaa matunda na ndipo alipotumia ubunifu huu.
"Mimi mwenyewe ni fundi wa magari, kwahiyo kazi ya kuunda na kuvisha bodi hili la mbao nilifanya mwenyewe," anasema.
Anasema baada ya matengenezo hayo gari hilo limekuwa kivutio kikubwa sehemu mbalimbali anazopita nalo.
"Sasa nalitumia kuhamasisha utalii, hasa utalii wa mazingira nikiwa na maana kwamba tukiyatunza mazingira yatatufaa kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na matengenezo ya magari kama hili langu," anasema.
Anasema gari hilo atalipeleka kwenye maonesho ya nanenane kama moja ya njia za kuhamasisha upandaji wa miti.
No comments:
Post a Comment