Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nchi ya Jamuhuri ya Kati haipaswi kuruhusiwa kugeuka kuwa Rwanda nyingine.
Akiandika maoni yake kwenye mtandao wa BBC,
Bwana Ban amesema kwamba zaidi ya nusu ya raia wa Jamuhuri ya Afrika ya
Kati wanahitaji msaada wa kibinadamu.
Akihusisha mambo yalivyo Jamuhuri ya Afrika ya
Kati na kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya halaiki nchini Rwanda,
amesema jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua sasa badala ya baadae
kuja kuomba msamaha itakapotimia miaka ishirini ijayo.
Siku ya Alhamis Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa liliwapa mamlaka wanajeshi 12,000 wa Umoja wa Mataifa waliopo
nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
No comments:
Post a Comment