Uchunguzi
Vipimo vya uchunguzi ambavyo hutumika katika kutambua tatizo la vidonda vya tumbo ni pamoja na kuangalia ndani ya utumbo ambavyo ni pamoja na kipimo kiitwacho Upper GI endoscopy au Gastroscopy.
Vipimo vya uchunguzi ambavyo hutumika katika kutambua tatizo la vidonda vya tumbo ni pamoja na kuangalia ndani ya utumbo ambavyo ni pamoja na kipimo kiitwacho Upper GI endoscopy au Gastroscopy.
Kwa kutumia kipimo hiki, daktari huangalia moja kwa moja ndani ya utumbo wa mgonjwa kuona sehemu iliyo na vidonda pamoja na ukubwa wa tatizo lake.
Vipimo hivi humuwezesha daktari kuchukua sehemu ya utumbo iliyoathiriwa kwa ajili ya kuchunguza zaidi maabara ili kutambua uwepo wa vidonda au tatizo jingine linalomsumbua mgonjwa tofauti na vidonda vya tumbo.
Kipimo kingine kijulikanacho kama Barium meal kina uwezo pia wa kuthibitisha uwepo wa ugonjwa wa vidonda vya tumbo.Vipo vipimo vingi sana vya kutambua uwepo wa uambukizi wa bakteria aina ya Helicobacter pylori kama vile kile kitwacho Urea breath test kipimo cha kuotesha kinyama kilichochukuliwa kutoka katika kipimo cha OGD (culture from an OGD biopsy specimen).
Kipo kipimo cha damu kwa ajili ya kutambua kiwango cha maambukizi ya vimelea wa H. pylori (antibody levels).
Kifupi ni kuwa kuna vipimo vingi sana kama vile cha kuangalia kiwango cha homoni ya gastrin katika damu, kuangalia kiwango cha tindikali inayozalishwa katika tumbo na kadhalika.
TIBA
Waliopimwa na kugundulika kuwa wana maradhi haya au bakteria wa H. pylori tiba inayotumika ni kuchanganya dawa za antibayotic (antibiotic) za aina tofauti kama Amoxicillin, Tetracycline, Clarithromycin au Metronidazole na dawa zenye uwezo wa kupunguza uzalishaji wa tindikali kwa wingi tumboni.
Mgonjwa anaweza kupewa nyongeza ya dawa na daktari iitwayo Bismuth compound.
Wale wagonjwa sugu, dawa za antibayotiki za aina tatu tofauti zinaweza kutumika ambazo ni Amoxicillin + Clarithromycin + Metronidazole ambazo hutumika sambamba na dawa yoyote moja kutoka kundi linalojulikana kitaalamu kama PPI kama vile Omeprazole au Pantoprazole pamoja na Bismuth Compound.
Wagonjwa wa kawaida wa vidonda vya tumbo ambavyo si sugu tiba bora inayoshauriwa ni kuchanganya dawa za antibibayotiki za aina mbili kama amoxycillin + metronidazole sambamba na dawa yeyote moja ya jamii ya PPI kama Pantoprazole.
No comments:
Post a Comment