Kumekuwa na kero mbalimbali pindi tunapoenda kwenye
ofisi mbalimbali kupata huduma katika ofisi hizo na hizi ndizo sababu
zinazofanya wafanya kazi wangi wasiwe makini na kazi walizopewa na waajiri wao.
Ø Mapenzi kazini;
Kiza hiki cha digital mapenzi yamekuwa wazi wazi na
sio kificho tena kama wazee wetu wazani walikuwa wanafanya mambo yao kwa siri
sana lakini hivi sasa vijana hawajali wapo wapi hata maofisini sasa wanatumia
kufanya uchafu wao haijalishi ni mfanyakazi mwenzake au kutoka nje ya ofisi.
Imefikia hatua wafanyakazi wanafanya mapenzi hata kwenye vyoo ya ofisi. Maofisini
sasa kumekuwa hakuna amani tena maana haijaalishi ni mke/mume wa mtu wote
wamekuwa ni wafuska tu.
Huko ndiko baadhi ya ndoa zimevunjika kutokana na
kusalitiana wakiwa kazini. Ndio maana wanaume wangine wanawaachisha kazi wake
zao baada ya kuona mienendo ya wake zao kuwa mibaya. Na baadhi ya maboss wa
siku hizi wamekuwa na tamaa sana kutembea na wafanyakazi wake kwa kuwa ahidi
kuwaongeza mshara au kuwapandisha cheo. Imekuwa kitu cha kawaida kwa wasichana
kutoa rushwa ya ngono ili kupata kazi kwa sasa kazi zimekuwa ngumu sana na
isitoshe kuna wanafunzi wengi ambao wanamaliza elimu ya juu na kutegemea
kuajiriwa.
Ø Utoro na Kutowajibika Ipasavyo;
Hili ndio janga la kitaifa hapa nchini kwetu kwani
utoro umekithiri sana ofisini. Wafanyakazi wangine wanakuja ofisini wana saini
na kuondoka na wangine muda wa lunch ukifika wakitoka kwenda kula ndio kimoja
mapaka kesho. Wafanyakazi hawaishiwi visingizio leo kafiwa na mama mkwe kesho
jirani kuna harobaini mara kuna mgonjwa hosipitali unataka kwenda kumuona yaani
nivisingizio mwanzo mwisho. Wafanyakazi wangine kutowajibika ipasavyo yani
atafanya kazi kidogo muda mwingine wote atalala kwenye meza yake mpaka muda wa
kuondoka akiulizwa atadai anaumwa najiskia vibaya.
Ø Umbea na Dharau kazini;
Siku hizi unaweza kuingia ofisi fulani ukakuta secretary
na mwenzie wanamsema mfanyakazi mwenzao hawajali kama wewe upo hapo dirishana
unasubiri wakupe huduma uliyofuata au kuapata maelekezo fulani watakuangalia
mpaka wamaliza umbea wao ndio wakusikilize shida yako. Kuna baadhi ya
wafanyakazi wanajisahau kufanya kilicho waleta nakujikuta wakitumia muda mwingi
kuwa sema wafanyakazi wenzao au watu wanaokuja kupata huduma kwenye ofisi hiyo
unaweza kukuta mtu hamfahamiani lakini anakuletea dharau kama ulimchukulia mume
wake na haswa hizi tabia wanazo sana wanawake hasa wale wanaokaa mapokezi.
Ø Mavazi yasiyo faa;
Wafanyakazi wa siku unaweza sema ni kizazi cha
swagga kwani wengi wao ni vijana tofauti na zamani mtu anamaliza chuo akiwa mtu
mzima lakini sasa ni watoto wadogo tu ndio wanao maliza chuo kwahiyo bado wana
akili za ujana wa kuvaa nguo fupi zakubana na kuonesha vifua vyao kwa kuacha
kufunga kifungo cha juu na wangine kuvalia suruali chini ya makalio. Wakiulizwa
wanakuwa wakali kama mbogo.
Ø Ulevi, Wizi, Matusi;
Unakuta asubuhi mfanyakazi amekuja ofisini na
mning’inio wapombe alizo kunywa jana usiku yani akiongea ananuka pombe utadhani
aliamkia bar ndio amekuja kazini. Ofisi zingine unakuta wanaitana majina kwa
matusi yani matusi ndio kiunganishi katika maongezi yao au unakuta mteja
anatukanwa na kujibiwa hovyo hovyo tu. Ofisi haieleweki yani ukiacha mzigo wako
kidogo tu haukuti wafanyakazi wamebeba.
Tubadilike watanzania kwa kuheshimu kazi uliyopata na
kuwajibika bila kutaka rushwa na kunyenyekewa kama wewe mfalme kumbuka kuna leo
kesho. Tufanye kazi kwa bidii na tupunguze utoro ili tukuze uchumi wa nchi yetu
na uchumi wa mtu binafsi.
No comments:
Post a Comment