KWA takribani wiki tatu sasa tumekuwa tukijadili kuhusu tabia ya baadhi ya walimu kujihusisha kimapenzi na wanafunzi, hasa wa kiume. Nashukuru kwamba nimepata mrejesho mzuri kutoka kwenu.
Lakini kuna mwalimu mmoja msomaji mzuri wa safu hii, yeye ni msichana anayefanya kazi mikoani. Alinitumia ujumbe mmoja ambao ulinivutia sana, nikabadilishana naye maneno mawili matatu na kujikuta nimepata kitu ambacho ni lazima tushirikiane pia kujadili.
Kwanza alinipongeza kwa makala ile, lakini baadaye akaniambia kuwa mara nyingi wanafunzi wa kike ndiyo wanaoanza kujitongozesha kwa walimu ambao wanachokifanya wao ni kama kumalizia tu.
Aliniambia kwamba wanafunzi wa kike wakiwa mbele ya walimu wa kiume hujishaua, wakati mwingine hata kupandisha juu sketi zao, kurembua macho na viuchokozi vingine ili mradi tu walimu wausome mchezo.
“Sasa anko kwa hawa walimu wenyewe vijana unategemea nini? Lakini ngoja tuwaite sisi walimu wa kike, wanakuja wamebetua midomo, wanaonyesha ishara ya dharau na vitu kama hivyo, mimi kwa kweli siwalaumu walimu, mara nyingi wanalazimishwa,” alisema mwalimu huyo.
Katika kukolezea na kuniaminisha anachokisema, alinipa mchapo mmoja unaomhusu yeye mwenyewe kiasi cha kuniacha hoi kabisa.
Aliniambia kuwa hapo awali, aliishi kinyumba na mwalimu mwenzake na walijaaliwa kupata mtoto mmoja. Kumbe jamaa kimya kimya akawa anajipigia kabinti kamoja ka darasa la sita hapo shule waliyokuwa wakifundisha. Dada akashtukia, ikawa bonge la msala. Huku na huku soo likafika kwa wazazi wa mtoto ambao nao hawakukubali, ikibidi sheria ichukue mkondo wake!
Polisi wakaipeleka mahakamani, kesi ikaanza kunguruma. Katikati ya shughuli, mtoto wa kike akatoa mpya. Akasimama mbele ya hakimu na wazazi wake, akawaambia kuwa yeye anampenda mwalimu, akawataka waachane na ile kesi na kama wataendelea nayo, atajiua!
Mchezo ukaishia hapo na dada yangu akaamua kumwachia mwanafunzi wake aendelee na mzigo, yeye akashusha manyanga!
Huo ni mfano ulio hai, lakini wanafunzi huko mashuleni wanaelewa zaidi. Ninakumbuka katika moja ya matoleo yaliyopita nilizungumzia kuhusu hili.
Wasichana wa aina hii mashuleni wako wa aina nyingi, lakini sana utakuta ni wale ambao hawana kitu kichwani au ambako kiasili ni wahuni. Mungu bwana wa ajabu sana, hawezi kuwanyima vyote wanadamu. Wasichana wasio na akili darasani hujaaliwa uzuri wa sura na umbo.
Nao hutumia uzuri wao kujiegemeza kwa walimu kwa mategemeo ya kusaidiwa mambo wanayoamini hawayawezi. Si rahisi kukuta mwanafunzi mwenye akili zake darasani na anayejua kitu alichokifuata shule, akambania pua mwalimu wake kwa lengo la kumteka kimapenzi.
Na kuna hawa wanafunzi vicheche wa asili, mtaani ana mabwana, shuleni anao, kwa ndugu zake anao ili mradi tu kila anapokwenda lazima apate mtu. Hawa ndiyo wanaoingia katika lile kundi la kujitongozesha, ingawa hata hivyo, wakati mwingine, mwanafunzi anaweza kumpenda mwalimu kama binadamu ye yote anavyoweza kufanya.
Labda niwaase maanko zangu kwamba pamoja na kuwa uhusiano wa kimapenzi haupendezi wakati ukiwa bado shule, hasa hizi za msingi na sekondari, ni vibaya zaidi kushiriki tendo hilo ovu na mwalimu wako.
Ni lazima tukubali kwamba kwa kufanya hivyo, moja kwa moja ni kwamba hakutakuwa na heshima baina yenu na hapa ndipo mkazo wa masomo kwa mwanafunzi unapowekwa kando. Mwalimu badala ya kumsisitiza mwanafunzi wake kujisomea, atataka muda ambao alistahili kuwa akijisomea, autumie kwa mambo yao ya mapenzi.
Nirudie tena wito wangu ambao nimekuwa nikiutoa kila mara. Tutumie vizuri muda wetu wa shule, tukiuchezea, tutakuja kushtuka muda umeenda. Haya mambo yote mnayotaka kuyafanya sasa, yapo, mtayakuta na kuyaacha.
No comments:
Post a Comment