Mmiliki wa kiwanda hicho, Lee Sliim, akiwa ndani ya gari la Polisi kuelekea kituoni kwa mahojiano zaidi.
Akielezea tukio hilo kwa waandishi wa habari jana, ndugu wa Jumanne aliyejitambulisha kwa jina la
Rehema
Rashid, alisema Novemba 17 mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku walipata
taarifa kuwa ndugu yake alipata ajali ya kukatwa mkono na mashine
kiwandani hapo.
Alisema
baada kupata ajali hiyo, Wachina hao kwa kusaidiana na wafanyakazi
wengine walimpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya
matibabu, ambapo ndugu wote waliendelea na huduma ya kumuuguza.
Mkono wa mtu uliopatikana kandokando ya Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Viroba na Plastiki, Mababi jijini Dar.
Rehema alisema jana wakiwa katika pilikapilika za kwenda kumjulia hali ndugu yao, walipata taarifa kwa wasamaria wema kwamba kiganja cha mkono wa ndugu yao kimeonekana kikiwa kimefukiwa pembezoni mwa kiwanda hicho.
“Leo
asubuhi tukiwa katika maandalizi ya kwenda kumwona Jumanne, tulipata
taarifa kutoka kwa wasamaria wema ambao wanafanya shughuli za kufua
vyuma chakavu karibu na kiwanda hicho wakitutaka twende kutambua kama
kiganja kilichofukiwa ni chake,” alisema Rehema
No comments:
Post a Comment