Akifungua semina ya majaji na viongozi wa juu wa
mahakama za haki za binadamu barani Afrika jana, Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda alisema Tanzania kwa sasa ni kati ya Serikali saba Afrika ambazo
zimeridhia viongozi wake kufunguliwa mashtaka ya haki za binadamu. Pia,
ni kati ya nchi 26 barani Afrika ambazo zimeridhia kuanzishwa Mahakama
ya Haki za Binadamu Afrika.
Hata hivyo, Pinda aliwataka majaji na watendaji wa
Mahakama za barani Afrika, kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa
kuzingatia misingi ya haki, taratibu na Sheria.
Alisema Tanzania itaendelea kuunga mkono Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika yenye makao makuu yake jijini hapa.
Awali, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande
Othman alisema semina hiyo ina umuhimu mkubwa kwa viongozi wa mahakama
kubadilishana uzoefu juu ya utendaji na kwamba, kuna mfumo unaofanana
katika kutafsiri sheria za masuala ya ukiukaji haki za binadamu.
Kuhusu mkataba wa kuwafungulia kesi viongozi wa
juu kwa ukiukaji haki za binadamu, Jaji Chande alisema taratibu
zimewekwa kwa kesi hizo kuanzia mahakama za kawaida za kila nchi kabla
ya kufikishwa Mahakama ya Afrika.
Naye Rais wa Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika,
Sophia Akuffo alitoa wito kwa nchi zote za Afrika kuridhia mikataba
mbalimbali ya haki za binadamu.
Pia, alitaka kutambua haki za binadamu kwenye nchi
hizo zinapaswa kuondoa upungufu katika katiba zao na kuondoa vitendo
vya ukiukwaji wa haki za binadamu.
mh. ametoa ya moyoni
ReplyDelete