Kanuni za kuepuka kuzini nje ya
Ndoa au mpenzi wako
Leo
tuende moja kwa moja kuangalia baadhi ya mambo ambayo yaweza kukusaidia kuepuka
kuzini nje ya ndoa yako au kutoweza kumsaliti mpenzi wako.
1. Kujiepusha kuwa karibu na jinsi zingine ukiwa umelewa
Hapa
nitoe ufafanuzi wa jambo moja la jinsi ambapo nazungumzia masuala ya maumbile
ambapo wengi wetu tunachanganya neno jinsi na Jinsia.
Kuepuka
kuwa karibu na jinsi tofauti nawe ni suala gumu sana lakini ni vema unapokuwa
unakula maji(kilevi) ni vema ukawa makini kuwa mbali na mtu wa jinsi nyingine
ili kuepukam kupata vishawishi na kumsaliti mwenzi wako.
2. Epuka mazungumzo ya kimahaba
Ni njia
rahisi sana inayoshawishi watu wengi kujiingiza kwenye usaliti ama mapenzi
mapya ambapo endapo hautakuwa makini na kujiingiza katika mazungumzo ya
kimahaba na mtu wa jinsi nyingine unaweza kujikuta unajiingiza katika usaliti
wa kimapenzi lakini nji hii licha ya kuwa ni njia moja wapo ya kuepuka usaliti
ni njia nzuri ya kuanzisha mapenzi mahusiano mapya ambapo wengi hushawishika na
kujikuta kutamani kupata vitu vipya katika mahaba ambavyo mtu aliyenaye kwa
muda huo amevigusa katika mazungumzo yao.
3.Kuwa mkweli
Ukweli
ni jambo muhimu katika kudumisha mahusiano na kuepuka usaliti kwasababu mwenzi
wako anaweza kuhisi kitu kuwa umeanzisha mahusiano na mtu mwingine ambaye mara
kadhaa mnafanya nae utani, hivyo ni vema ukawa mkweli kwa mwenzi wako kumweleza
kuwa mtu huyo mnafanya masihara nae na wala hakuna jambo lolote linaloendelea
kimahusiano tofauti na kutumia lugha kama ‘’Kwani unafikiri mimi nafanya nini
nae’’ hilo jibu sahihi katika kuboresha mahusiano yenu.
4.Epuka kupigana busu na jinsi
nyingine
Kumpiga
busu mtu ambaye si jinsi moja nawe ni kichocheo cha usaliti katika ndoa na hata
mapenzi ya kawaida kwasababu Mungu aliumba miili yetu katika misisimuko ya aina
mbalimbali ambapo mtu mwingine ukimpiga busu bila kujalisha kuwa ni mwanaume au
mwanamke hujikuta anasisimuka vibaya sana na kuhisi kuwa angekuwa sitakwa sita
nawe kwa muda huo angesisimuka hivyo si vema kufanya hicyo.
5. Usimweleze mtu hisia zako
Epuka
kueleza hisia zako za kimahaba kwa mtu asiye wa jinsi yako kwa mfano mtu
kagombana na mpenzi wake ama mke/mume wake si vema ukamwambia hisia zako kwake
za kutomtenda bali ni vema kumwambia kuwa siyo vizuri kugombana na mwenzi wake
na jaribu kutoa ushauri ambao hauna ushawishi wa kumwondoa kwa mwenzi wake.
Hapa
sielezi kuwa haupaswi kuwa mkarimu kwa watu la hasha bali nazungumzia kuwa
makini na kuepuka kuwa mmoja wa watu wenye historia za kuvunja mahusiano ya
watu bali ukiwa mshauri mwema utaheshimika zaidi.
6. Onyesha wajibu wako
Ni vema
katika mahusiano kila upande ukaonesha wajibu wake kwa mwenza wake ambapo
waweza kumtia moyo mwenzi wako kuwa yeye amekuwa sumaku kwako kwa kukupa faraja
na hasa ni mwanamke/Mwanaume ambaye
ulikuwa ukitamani siku nyimgi kuwa naye na hatimaye Mungu kakupa macho ya
rohoni kumpata yeye.
Hapa
wapo baadhi ya watu ambao si wakweli ambao wanafanya maigizo kutamka maneno
kama haya huku wakitoa zawadi ili kuficha mambo yao huo ni usaliti na hapa nasema kuwa
haifai….kama upo hivyo jirekebishe acha usaliti.
Mpenzi
msomaji wa safu hii ya Hakunaga baada ya kuoina baadhi ya njia ambazo zinzweza
kukusaidia kutojiingiza katika usaliti wa mapenzi na ndoa wiki ijayo tutaona nji
kadhaa wanazoweza kuzitumia wanawake kuwa sumaku kwa wanaume wao.
No comments:
Post a Comment