Awamu
ya pili ya Tanzania kuhamia kwenye matangazo ya mfumo wa dijitali
inatarajia kuanza mwakani, ambapo mikoa iliyosalia itahama kutoka
analojia kwenda dijitali.
Mkurugenzi
Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania Profesa, John Nkoma alikuwa
akiongea kwenye maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa mamlaka
hiyo na kuelezea ratiba hiyo.
Mpaka
sasa makampuni ya StarTimes Media Limited, Basic Transmission na Agape
Associates Limited ndiyo yanayohusika na utoaji wa huduma ya matangazo
hayo.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Makame Mbarawa, alisema ndani ya
miezi mitatu hadi minane mikoa mingine itahamia dijitali pia.
No comments:
Post a Comment