KUKU WA AJABU ATUA OFISINI AKIWA NA HIRIZI SHINGONI
AJA NA UJUMBE WENYE ONYO KALI
AJA NA UJUMBE WENYE ONYO KALI
KUKU AKIWA AMETUA NA UJUMBE HUO.
WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Reli, kati ya Tanzania na
Zambia(TAZARA) jana walijikuta katika wakati mgumu na baadhi yao kulazimika
kuzikimbia ofisi zao, baada ya ndege aina ya njiwa kukutuwa katika moja ya choo
cha ofisi hiyo akiwa amefungwa hirizi shingoni, huku akiwa na barua yenye
ujumbe wa onyo kali.
Tukio hilo la aina yake, lilitokea mapema leo
saa mbili asubuhi katika ofisi za mamlaka hiyo zilizopo eneo la
Iyunga Mkoani mbeya, hali ambayo mbali na baadhi ya wafanyakazi wake kuzikimbia
ofisi, ilisababisha kuibuka kwa mjadala mkubwa dhidi ya tukio hilo.
Mtandao huu ulifanikiwa kushudia njiwa huyo
mweusi akiwa nyuma ya choo cha kiume katika eneo hilo la ofisi ya
mwajiri, huku akiwa amefungwa hirizi shingoni iliyozungushiwa shanga
mchanganyiko wa rangi tatu, ambazo ni Nyekundu, Njano na Nyeupe.
Mbali ya kuwa na hirizi hiyo, pia njiwa huyo alikuwa
amebeba barua inayodaiwa kuwa ni ya mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo (jina
limehifadhiwa kwa sababu maalumu) ambaye anadaiwa hivi karibuni kufukuzwa kazi
kwa makosa ya ubadhirifu.
Barua hiyo ilikuwa na maandishi mekundu yenye ujumbe
ulioandikwa kwa lugha mbili za Kiswahili na kiarabu, ambapo katika maandishi ya
Kiswahili yalisomeka “ Naomba majibu haraka kama mtarudisha binti huyu kazini”
ilisema sehemu ya ujumbe huo, huku ikiwa na orodha ya majina matatu ya viongozi
wa shirika hilo.
Mbali na ujumbe huo ukiwa umeandikwa kwa maandishi
ya mkono yaliyokolezwa kwa wino mwekundu upande wa nyuma, lakini upande wa
mbele kulikuwa na maandishi yakiwa ni barua ya kutaarifiwa kufukuzwa kazi kwa
mfanyakazi huyo.
Akizungumzia tukio hilo, Mwajiri wa mamlaka hiyo
kanda ya Mbeya, aliyejitambulisha kwa jina la Mchaba Mgweno, alikiri kutokea
kwa tukio hilo na kwamba waliobaini ni wahudumu wa usafi.
Aliongeza kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo
aliwaarifu na wafanyakazi wenzake ambao walikusanyika na kumshuhudia Njiwa huyo
mweusi akiwa amedhoofika huku akiwa na barua hiyo yenye vitisho.
Alisema baada ya kushuhudia hali hiyo waliamua kutoa
taarifa kituo cha polisi kilichopo ndani ya shirika hilo, ambapo waliichukua
barua hiyo na baadhi ya wafanyakazi hao wakienda kutoa maelezo kituoni hapo.
“Kwa kweli hali hii si ya kawaida, ila kwa sasa
siwezizungumzia chochote kwa kuwa hata mimi tukio hili limeniweka katika wakati
mgumu na nimeshindwa kuendelea na majukumu yangu ” alisema Mgweno.
Hata hivyo kuliibuka malumbano makali kati ya
wafanyakazi wa shirika hilo walioshuhudia tukio hilo, ambapo baadhi yao wakidai
kuwa tukio hilo ni la kutengenezwa kwa lengo la kuchafuana.
“Hebu angalia hiyo barua yenyewe mbona ni kivuli
(Photocopy), kama ingekuwa ni ya ….wanamtaja mfanyakazi aliyefukuzwa jina
limehifadhiwa ingekuwa ni nakala halisi….haiwezekani mambo haya ni kutaka
kuchafuana tu” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.
Lakini baadhi yao wakiamini kweli kuwa barua hiyo
ilitumwa ili itoe vitisho kwa viongozi wa shirika hilo.
Baadhi ya askari polisi wa kituo cha Tazara walikiri
kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli
wake.
“Ndugu zangu nyie mnajua taratibu za utoaji wa
taarifa kwa jeshi hili, maana wapo wahusika, lakini kwa kifupi sisi tulipokea
taarifa na tunaendelea kuzifanyia kazi” alisema mmoja wa askari hao.
Hata hivyo,
hadi tunapoondoka eneo la tukio majira ya saa sita mchana Njiwa huyo alikuwa
bado yupo eneo la tukio.
Chanzo: Mbeya yetu
Chanzo: Mbeya yetu
OFISI YA TAZARA MBEYA
Njiwa akiwa amedhoofu kwa Baridi akiwa katika choo cha wanaume
Hii ni sehemu alipokutwa Njiwa huyo
Majengo nje ya Ofisi ya Afisa Mwajiri
Baadhi ya wafanyakazi wakielekea eneo la tukio
Afisa Mwajiri (Mwenye shati ya bluu) Na baadhi ya wafanyakazi wakishuhudia tukio
Mashuhuda wakitoka eneo la tukio
Barua iliyoletwa na Njiwa maeneo ya Ofisi ya Mwajiri upande wa mbele na nyuma
Jengo la Ofisi ya Afisa Mwajiri
No comments:
Post a Comment