Mwili wa
binadamu waweza pia kufananishwa na nyumba kwasababu nyumba ili ikamilike
inahitaji uuwepo wa matofali,mchanga, simenti na malighafi nyingine nyingi na
inahitaji ukarabati wa mara kwa mara ili iweze kuwa nyumba bora.
Watu husema
kuwa mwili haujengwi na matofali bali kwa vyakula vitatakavyo uwezesha mwili
katika utendaji wa kazi mbali mbali lakini pia mazoezi ya viungo ili kufanya
mwili kuwa imara zaidi na wenye nguvu. Mwili wa binadamu unapokosa mazoezi ya
kutosha hufanya mwili kunyong’onyea na fufanya baadhi maeneo katika mwili
kushindwa kufanya kazi vizuri kama inavyotakiwa.
Mazoezi ya mara kwa
mara au kufanya kazi zinazohusisha matumizi ya nguvu ya mwili yanasaidia mifumo
mingi ya mwili kufanya kazi inavyotakiwa, mazoezi yatatuepusha na magonjwa ya
moyo, kisukari, na hata magonjwa mengine hayataweza kushambulia miili yetu, na
ni njia nzuri ya kupunguza uzito wa mwili uliozidi. Unapokuwa unafanya mazoezi
mara mara utafaidika na mambo yafuatayo:
![]() |
Mwanamke akifanya mazoezi ya viungo. |
Moja ni kuongeza nafasi
ya kuboresha umri wa kuishi na kuishi katika afya njema.
Pili mazoezi
yanasaidia kutulinda na kutuepusha na magonjwa nyemelezi kama homa na magonjwa ya
moyo na magonjwa yanayoambatana nayo kama shinikizo la damu na ongezeko au
kiwango cha juu cha damu katika mwili. Kiwango cha juu cha damu katika mwili
kimekuwa kisababishi cha ongezeko la shinikizo la damu na hata kuwa katika
hatari ya kupata kiharusi.
Tatu mazoezi
yanatusaidia kuepukana na magonjwa ya kansa kama kansa ya tumbo, kansa ya matiti, kansa ya
mapafu na kansa ya kizazi. Hii ni kwa sababu mazoezi yanaboresha mifumo mbali
mbali ya mwili na kuwezesha mwili kutoa taka na sumu mbali mbali mwilini,
pamoja na kuimarika kwa kinga ya asili ya mwili.
Nne mazoezi husaidia
kuongeza uwezo wa kuona mbali hasa kwa wazee na watu watu wa makamo lakini kwa
sasa tatizo hili linawakumba mpaka vijana kwa sababu vijana wengi hawafanyi
mazoezi
Pia mazoezi yanasaidia
kutukinga na kisukari aina ya pili (ugonjwa ambao mtu anaupata ameshakuwa
mkubwa na sio kwa kuzaliwa), na kutukinga na matatizo ya mmeng’enyo ambayo
yanaweza kutuletea magonjwa ya moyo na kisukari pia.
Mazoezi husaidia kuimarisha
afya ya akili, yanasaidia kutuepusha na magonjwa ya kupoteza kumbukumbu hasa
kwa wazee. Pia mazoezi yanatuondolea msongo wa mawazo, woga na mtu kuwa katika
afya nzuri ya akili.
Mazoezi yanasaidia
kuwa na mapafu yenye kufanya kazi vizuri,moyo wenye afya na kuimarisha misuli
ya mwili kwa ujumla. Bila kusahau kuwa mazoezi husaidia kupata usingizi mzuri
kwa afya bora.
Mazoezi ni sehemu muhimu ya kuzingatia katika kuujenga na kuulinda mwili wako ili usikumbwe na magonjwa na matatizo yatakayo ufanya mwili kudhoofu katika utendaji wa kazi mbali mbali katika mwili.
No comments:
Post a Comment