Maskini!
Dereva wa pikipiki ya abiria maarufu kama bodaboda jina halikunaswa
mara moja kwa kuwa alikuwa hawezi kuzungumza amepata ajali mbaya na
kuvunjika mguu wa kulia kisha kukatika vidole vitatu vya mkono wa kulia.
Muonekano wa pikipikibaada ya ajali.
Tukio hilo lilitokea juzi mara baada ya jamaa huyo kugongwa na lori
la mchanga katika eneo la Daraja la Mkolani wilayani Nyamagana nje
kidogo ya Jiji la Mwanza.
Amepata ajali mbaya na kuvunjika mguu wa kulia kisha kukatika vidole vitatu vya mkono wa kulia.
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio, baada ya jamaa huyo
kuumia vibaya, wasamaria wema walijitokeza na kumkimbiza kwenye
Hospitali ya Rufaa ya Bugando.
Habari zilieleza kuwa dereva huyo alikuwa akitokea maeneo ya Mkolani
kuelekea Buhongwa ambapo lori lililomgonga lilikuwa Buhongwa kuelekea
Mkolani.
Ilidaiwa kuwa dereva wa lori ‘aliovateki’ daladala iliyokuwa mbele
yake na baada ya kuipita ndipo akakutana uso kwa uso na bodaboda.
No comments:
Post a Comment