TTCL

EQUITY

Wednesday, October 9, 2013

DULLY SYKES ATOA KAULINZITO KWA DIAMOND


Msanii wa longtime kwenye familia ya bongofleva ambae mwenyewe anajiita mwanzilishi wa bongofleva, Dully Sykes, ameweka wazi kwamba kamwe hawezi kuwa adui na wasanii wapya kwenye muziki huu.

Dully ambae ni miongoni mwa wasanii waliowahi kumiliki chati za muziki kutokana na hits nyingi, amesema inaumiza anaposikia kuna msanii mkubwa hapendi kuwaona wala kuwasikia wasanii wapya wa bongofleva.
Anasema ukaribu wake na wasanii wapya ndio unamuwezesha yeye kuendelea kuwepo kwenye muziki kwa sababu wasanii wapya ndio wanaomiliki mawimbi kwa wakati huu.

Akimzungumzia Diamond Platnums ambae hana hata miaka mitano toka aanze kung'aa, Dully anakwambia watu kama Diamond ndio wamefanya hata na wasanii wengine waanze kulipwa mamilioni kwenye show kutokana na msimamo wake.
“Sipendi kuona mtu akiwachukia hawa, sisi tumeshazeeka ila hawa ndio wakati wao na mimi nitaendelea kuwa karibu yao siku zote.... Wasanii wakongwe waache wivu muda umepita,” asema Dully.

Inaaminika Diamond Platnums ambae ndio anashikilia rekodi ya kuwa msanii anaefanya showz nyingi zaidi huku bei yake ikiwa ni milioni 10 kwa show ya Tanzania, amekua akichukiwa na wasanii wengi wa bongofleva kutokana na rekodi anayoivunja sasa hivi, ikiwemo kupata dili na makampuni makubwa kama Vodacom, Cocacola na mengine.

No comments:

Post a Comment