Askari Polisi wa kike mkoani hapa amefariki dunia papo hapo baada ya kukanyagwa na tairi la gari na kupasuka kichwa.
Askari huyo Rehema James (30), alikutwa
na umauti juzi wakati akiwa amepanda katika usafiri wa baiskeli maarufu
kama daladala eneo la Kambarage mjini Shinyanga.
Watu walioshuhudia tukio hilo waliliambia
gazeti hili kuwa, askari huyo alikuwa amepakizwa kwenye baiskeli ndipo
gari hilo lilipomgonga na kufariki dunia.
Walisema waliona gari aina ya scania lenye
namba za usajili BLQ 546 likimgonga askari huyo na kufariki dunia papo
hapo na ubongo wake ukiwa nje huku mwendesha baiskeli akifanikiwa
kuruka kutoka kwenye baiskeli hiyo na kukimbia.
Walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni
mwendesha baiskeli kutaka kulipita gari hilo wakati likikata kona na
Rehema alijigonga kwenye tela la gari na kuanguka chini ambapo tairi
lilimpitia na kumpasua kichwa.
Utingo wa gari hilo, God Makunga, alisema
wakati gari lao likikata kona ghafla alisikia kishindo kikubwa kwenye
gari na baada ya kushuka akamkuta mwanamke huyo amekanyangwa na tairi
la gari.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Alisema Rehema alikuwa abiria kwenye
baiskeli na baadaye akagongwa na gari hilo, na tayari mwili wake
umesafirishwa kwenda nyumbani kwao jijini Dar es Salaam kwa mazishi
yanayotemewa kufanyika leo.
Alisema chanzo cha ajali hiyo
kinachunguzwa na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta dereva wa gari
hilo kwani alitoroka mara baada ya ajali kutokea na kuacha gari lake
eneo la tukio.
Kamanda Kihenya ametoa wito kwa watumiaji
wa barabara wakiwamo madereva wa magari na waendesha baiskeli kuwa
makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/08/inatisha-askari-wa-kike-afariki-dunia.html#ixzz2b8HiCJd2
No comments:
Post a Comment