Jeshi lashika nchi; Lasimamisha Katiba
Rais Mohammed Morsi wa Misri aliyechaguliwa kwa njia za demokrasia amepinduliwa na jeshi la nchi hiyo na Katiba ya nchi hiyo imesitishwa huku jeshi likimteua Jaji wa Mahakama ya Katiba kuwa Mkuu wa Muda wa Nchi. Akizungumza katika televeshini Mkuu wa Jeshi la Nchi hiyo Generali Abdel Fattah Al-Sisi amesema kuwa jeshi la nchi hiyo haliwezi kuiacha Misri ikiwa katika hali ya kuyumba na mgongano wa kisiasa usiokwisha na hivyo ili kulinda maslahi ya watu wa Misri na taifa lao jeshi limeamua kuchukua nchi. Habari hizo zimesababisha mlipuko wa shangwe kwa maelfu – kama siyo mamilioni – ya wananchi wa Misri ambao walikuwa wamekusanyika kwa siku kadhaa sasa katika viwanja vya Tahrir ambao walikuwa wanasubiria habari hii kwa shauku kubwa.
Gen al-Sisi akizungumza kwenye Televisheni
Wanajeshi wakisimama kulinda Makao Makuu ya Kikosi Maalum cha Ulinzi wa Rais
No comments:
Post a Comment