Gharama ndogo za simu kuongeza masoko na wateja
MKAZI wa jijini Dar es Salaam, Hija Omar
analazimika kutumia wastani wa Sh5,000 kwa siku kwa ajili ya mawasiliano
ya simu kutokana na kipato chake. Omar anafanya ya kuuza matairi ya
pikipiki ya magurudumu matatu.
Bila kufanya hivyo anaweza kupoteza wateja wake
ambao wanategemea chombo hicho kuwafikisha maeneo ya katikati ya Jiji la
Dar es Salaam ambako teksi haziwezi kufika kirahisi.
Omar ana kazi zaidi ya moja na mitandao mitatu tofauti ya simu za mkononi inayomsaidia kuwasiliana na wateja wake.
“Ninakwepa gharama za kuwasiliana, wateja wangu
ambao wapo mitandao tofauti , siwezi kutumia laini ya voda au Airtel
kuwasiliana na mteja wa Tigo.
“Hata kama mtu ‘akinibipu’ ni rahisi kumpigia hii
ndiyo sababu nalazimika kutumia laini zaidi ya mbili,” anasema dereva
huyo wa Bajaj.
Kadhia ya kuwa na laini zaidi ya moja inayomsibu
Hija huenda ikamalizika kesho, baada ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini
(Tcra) kushusha gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda
mwingine. Tcra imeshuka gharama za siku kutoka Sh115 mpaka Sh34.92 kwa
dakika moja.
Hii ni habari njema kwa Hija na watumiaji wengine
wa simu za mkononi ambao kwa mujibu wa taarifa za Tcra mpaka kufikia
Septemba, mwaka jana kulikuwa na watumiaji wanaokadiriwa milioni 23.8
waliosajiliwa sawa na asilimia 93 ya watumiaji wote waliosajiliwa kutoka
kampuni saba za simu za mkononi nchini.
Tcra ilifanya mabadiliko hayo baada ya kupitia gharama za mwingilio wa kampuni za simu na kuweka punguzo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tcra, Profesa John Nkoma
anasema wameshusha gharama hizo ili watumiaji wa simu wawe huru kupiga
simu kwenda mtandao wowote.
Anasema gharama mpya zitawaondolea Watanzania mzigo wa kubeba laini nyingi za mitandao tofauti.
Profesa Nkoma anasema uamuzi wa kushusha gharama
za mwingiliano wa mawasiliano ya simu za mkononi itakuwa sheria ambayo
kampuni zote za simu zitalazimika kuzitekeleza.
No comments:
Post a Comment