TTCL

EQUITY

Tuesday, May 10, 2016

Tanzania yawasilisha ripoti ya Haki za Binadamu UN

Tanzania imewasilisha leo ripoti yake ya miaka minne ya utekelezaji wa haki za binadamu kwa Umoja wa Mataifa mjini Geneva nchini Uswisi, ambapo imeeleza kupiga hatua katika maeneo kadhaa ikiwamo elimu.
 
Mwakilishi wa Kudumu wa nchi Tanzania, katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Balozi Modest Mero,(kulia). 
 
Mwakilishi wa kudumu wa nchi Tanzania, katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Balozi Modest Mero, amesema licha ya changamoto kadhaa za ukosefu wa fedha amesema serikali ya Tanzania imetekeleza karibu asilimia 50 ya maelekezo kama walivyoshauriwa katika ripoti ya awali.

Balozi Mero amesema kuwa katika ripoti hiyo imeonyesha changamoto nyingine ambazo zimefanywa kushindwa kufikia malengo kamili kutokana na kushindwa kuridhia baadhi ya sheria za Kimataifa ambazo zinakinzana na sheria za ndani ya nchi.

Kuhusu mjadala wa kuminya haki ya mawasiliano kufuatia kupitishwa sheria ya mtandao nchini Tanzania, Balozi Mero amesema kuwa sheria hiyo ipo duniani kote kutokana na malengo yake makuu ikiwemo kuzuia uhalifu ikiwemo ugaidi na matukio mengine ya uvunjifu wa amani.

No comments:

Post a Comment