TTCL

EQUITY

Tuesday, March 1, 2016

Wauguzi sita Temeke wasimamishwa kwa kuuza gloves

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Hamis Kigwangala leo ameagiza wauguzi sita wasimamishwe kazi kwa kutuhumiwa kuuza mipira ya kuvaa mikononi ya kujikinga (gloves) kwa wanawake wajawazito katika hosipitali ya Temeke.

Dkt. Kigwangala ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Temeke, kujionea utendaji wa wafanyakazi wa hospitali hiyo.
Aidha, Dkt. Kigwangala amesema hatua hiyo anaichukua kwa makusudi ili kuwa fundisho kwa wauguzi wote nchini ambao wamekuwa wakiikwamisha serikali katika jitihada za kukabiliana na vifo vya wakina mama wajawazito na watoto.

No comments:

Post a Comment