TTCL

EQUITY

Wednesday, March 2, 2016

Tanzania kuitumia SADC kukomboa wananchi kiuchumi

Serikali ya Tanzania ina mpango wa kushirikiana na nchi za SADC ili kuwakomboa wananchi wake kiuchumi kupitia uwekezaji.
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imesema Tanzania kwa sasa inashirikiana na nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo nchi za Kusini mwa Afrika SADC, katika kutekeleza mkakati wa kuwakomboa wananchi wake kiuchumi baada ya kufanikiwa kwa juhudi za ukombozi katika nyanja ya kisiasa....
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Adolf Mkenda, amesema hayo leo katika siku ya kwanza ya mkutano wa kimataifa unaozikutanisha taasisi zinazohusika na ukuzaji wa uwekezaji kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC, mkutano unaofanyika jijini Dar es Salaam chini ya uenyeji wa Kituo cha Uwekezaji nchini TIC
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Bi. Juliet Kairuki amesema kituo chake kwa sasa kinakamilisha mfumo maalumu utakaopunguza mlolongo na taratibu ndefu za uwekezaji ambapo mwekezaji anaweza kupata leseni ya uwekezaji ndani ya kipindi kisichozidi siku tano kutoka wastani wa sasa wa siku kumi na mbili

No comments:

Post a Comment