TTCL

EQUITY

Monday, March 14, 2016

MUSHI; TUMEJIPANGA KUTATUA KERO ZOTE ZA UALIFU NA TAYARI TUMELIPATIA TATIZO UFUMBUZI.

serikali ya mtaa yajipanga kudhibiti wizi unaotumiwa na bodaboda

Mwenyekiti wa mtaa wa Themi Mashariki Mh. Godfrey Mushi mapema leo akizungumza na mwandishi wetu (hayupo pichani) alipotembelea ofisini kwake. 

Uongozi wa serikali ya mtaa wa Themi mashariki umesema kuwa, wamepokea malalamiko mengi ya matukio ya unyang'anyi na uporaji kwa kutumia usafiri wa bodaboda, na wao kama serikali wamekwisha jipanga namna ya kuhakikisha wanavalia njuga suala hilo la uporaji na kuhakikisha linakoma na wahusika wake wanapatikana mara moja.


baadhi ya Madereva wa bodaboda na viongozi wa serikali ya mtaa wakijadiliana namna ya kudhibiti wezi wanao tumia usafiri wa bodaboda kuibia watu na wakati mwingine kuwaachia majiraha
Akizungumza mapema ofisini kwake alipotembelewa na mwanahabari wetu Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Themi mashariki Mh. Godfrey Mushi ameeleza kuwa serikali yake imekuwa na mkakati wa muda mrefu wa kuhakikisha inawapata vijana wa kufanya kazi ya ulinzi shirikishi, ambapo mwaka jana waliandaliwa vijana kadhaa na wakapata nafasi ya kushiriki mafunzo ya mgambo na baadae kushiriki mbio za kijeshi ambapo baada ya ujio wa Mh. Rais katika shughuli ya kuwapandisha vyeo askari wa Jeshi la wananchi JWTZ, miongoni mwa waliopata ajira kwa wito wa Mh. Rais, vijana hao walikuwa ni miongoni mwao waliopata fursa ya ajira katika jeshi la wananchi JWTZ, hivyo yeye pamoja na wajumbe wa serikali ya mtaa wamekwishafanya usahili mwingine na sasa wapo katika hatua za mwisho za kuwakabidhi kazi.
"Polisi jamii (ulinzi shirikishi) wapo imara na timu hii inaundwa na askari wa staafu wa jeshi la polisi, mgambo, pamoja na vijana wengine wa mtaa wetu wa Themi mashariki". Pia amelalamikia Jeshi la polisi kwakutoonesha ushirikiano, na kuunga mkono juhudi za serikali ya mtaa katika kuunda kikosi cha ulinzi na usalam wa mtaa, "Mwaka jana Polisi tuliwaomba waje kutoa mafunzo elekezi kwa vijana wetu wa polisi jamii lakini hawakufika kabisa, na hakuna aliyekuwa tayari kutolea ufafanuzi wa kwanini shughuli hii ili kwama. hivyo naweza kusema kuwa kwa kiasi kikubwa wao pia walichangia zoezi hili kutokukamilika mnamo mapema" alisema.
Aidha alieleza kuwa, baada ya taratibu zote kukamilika anategemea mapema tarehe moja mwezi Aprili mwaka huu 2016 kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama watakuwa wamekamilisha taratibu zote na Polisi jamii wataanza kazi rasmi.

No comments:

Post a Comment