TTCL

EQUITY

Thursday, February 11, 2016

NICK‬ VUJICIC; MLEMAVU MWENYE MAFANIKIO MAKUBWA DUNIANI

  • Alimuomba Mungu miguu mikubwa na mikono, akanunua viatu kuamini atapata miguu
  • Alipoona hapati akamshukuru Mungu kwa uhai alionao.
Unakuwa miguu, na unakimbia kwa kasi huku ukirukaruka. Unakuwa na mikono, unashika kila kitu unachotaka kushika. Mungu amekupa viungo vyote, haimaanishi wewe ni muhimu kuliko walemavu wengine, jua kwamba ni nafasi ya kipekee na ya upendeleo uliyoipata, inawezekana haukustahili.
Kwa jina anaitwa Nicholas James "Nick" Vujicic, ni miongoni mwa watu waliofanikiwa japokuwa hana mikono, na miguu aliyokuwa nayo ni midogo mno. Leo, unapozungumzia kuhusu watu wenye mafanikio ambao ni walemavu, basi jina lake litakuwa miongoni mwa majina hayo.
Mbali na ulemavu aliokuwa nao lakini Vujicic ni mfundishaji mzuri kwa watu masomo na mbinu zinazoweza kumfanya mtu kufanikiwa (motivational speaker). Katika kila semina anayoifanya, watu wengi wanakusanyika na kumsikiliza huku, wanajifunza mbinu za kufanikiwa kutoka kwa mtu ambaye wala hawezi kukimbia.
Azaliwa akiwa na Phocomelia
Vujicic alizaliwa mwaka 1982 katika Jiji la Melbourne nchini Australia. Mara baada ya kuzaliwa, madaktari walipomuona, walishtuka kwani aligundulika kuwa na tatizo la kukosa viungo ambalo kwa kitaalamu huitwa Phocomelia.
Alipokuwa akikua, hakutaka kujiona kama alikuwa mlemavu bali alichokifanya ni kufanya mazoezi kwa nguvu, kuvipa nguvu viungo vyake hasa miguu yake ambayo ni midogo mno isiyokuwa na uwezo hata wa kuvalishwa viatu.

SAFARI YAKE YA MASOMO
Alianza kusoma katika Shule ya Runcorn State ambayo ipo nchini Australia inayochukua watoto kuanzia miaka 12-17. Alipofikisha miaka 17, akaanza kuzungumza na wanafunzi mbalimbali akiwafundisha kuhusu mafanikio, nini walitakiwa kufanya, nini hawakutakiwa kufanya ili wafanikiwe.
Alipofikisha miaka 21, akamaliza masomo yake katika Chuo cha Griffith na kuchukua Shahada ya Uchumi, pia akachukua Uhasibu na Mipango Fedha kwa pamoja.
Mafundisho yake yaliwavutia watu wengi na hivyo kukusanyika na kuanza kumsikiliza. Wengi walimtabiria mafanikio hapo baadaye, hakuacha kujifunza, ili kuwa mwalimu mzuri ilikuwa ni lazima mtu ajifunze, hivyo akafanya hivyo.
• Alimuomba Mungu miguu mikubwa na mikono, akanunua viatu kuamini atapata miguu
• Alipoona hapati akamshukuru Mungu kwa uhai alionao.
Unakuwa na miguu, unakimbia kwa kasi huku ukirukaruka. Unakuwa na mikono, unashika kila kitu unachotaka kushika. Mungu amekupa viungo vyote, haimaanishi wewe ni muhimu kuliko walemavu wengine, jua kwamba ni nafasi ya kipekee na ya upendeleo uliyoipata, inawezekana haukustahili.
Kwa jina anaitwa Nicholas James "Nick" Vujicic, ni miongoni mwa watu waliofanikiwa japokuwa hana mikono, na miguu aliyokuwa nayo ni midogo mno. Leo, unapozungumzia kuhusu watu wenye mafanikio ambao ni walemavu, basi jina lake litakuwa miongoni mwa majina hayo.
Mbali na ulemavu aliokuwa nao lakini Vujicic ni mfundishaji mzuri kwa watu masomo na mbinu zinazoweza kumfanya mtu kufanikiwa (motivational speaker). Katika kila semina anayoifanya, watu wengi wanakusanyika na kumsikiliza huku, wanajifunza mbinu za kufanikiwa kutoka kwa mtu ambaye wala hawezi kukimbia.
Azaliwa akiwa na Phocomelia
Vujicic alizaliwa mwaka 1982 katika Jiji la Melbourne nchini Australia. Mara baada ya kuzaliwa, madaktari walipomuona, walishtuka kwani aligundulika kuwa na tatizo la kukosa viungo ambalo kwa kitaalamu huitwa Phocomelia.
Alipokuwa akikua, hakutaka kujiona kama alikuwa mlemavu bali alichokifanya ni kufanya mazoezi kwa nguvu, kuvipa nguvu viungo vyake hasa miguu yake ambayo ni midogo mno isiyokuwa na uwezo hata wa kuvalishwa viatu.

SAFARI YAKE YA MASOMO
Alianza kusoma katika Shule ya Runcorn State ambayo ipo nchini Australia inayochukua watoto kuanzia miaka 12-17. Alipofikisha miaka 17, akaanza kuzungumza na wanafunzi mbalimbali akiwafundisha kuhusu mafanikio, nini walitakiwa kufanya, nini hawakutakiwa kufanya ili wafanikiwe.
Alipofikisha miaka 21, akamaliza masomo yake katika Chuo cha Griffith na kuchukua Shahada ya Uchumi, pia akachukua Uhasibu na Mipango Fedha kwa pamoja.
Mafundisho yake yaliwavutia watu wengi na hivyo kukusanyika na kuanza kumsikiliza. Wengi walimtabiria mafanikio hapo baadaye, hakuacha kujifunza, ili kuwa mwalimu mzuri ilikuwa ni lazima mtu ajifunze, hivyo akafanya hivyo.

 MAFANIKIO‬ YAKE
Mwaka 2005 akatoa DVD yake ya masomo iitwayo Life's Greater Purpose (Dhamira Kubwa Zaidi Katika Maisha) ambayo ilikuwa katika mtindo wa makala. Mbali na hiyo DVD yake ya pili aliifanya kwenye kanisa alilokuwa akisali lililopo Brisbane huko Australia aliyoiita No Arms, No Legs, No Worries (Hakuna mikono, Hakuna Miguu, Hakuna Mashaka).
Mbali na DVD hizo pia alishiriki katika filamu mbalimbali kama The Butterfly Circus (2010) ambapo alishinda Tuzo ya The Feel Good Film Festival huko Holywood nchini Marekani.
Mwaka 2010 akaandika kitabu chake alichokiita Life Without Limit: Inspiration for a Ridiculously Good Life (Maisha Bila Kikomo: Matumaini Kwa Maisha Mema ya Mzaha.

Kevin Lameck's photo.

MAISHA YAKE YA NDOA
Vujicic amemuoa mwanamke aitwaye Kanae Miyahara mwaka 2012 ambaye amezaa naye watoto wawili, Kiyoshi James (2013) na Dejan Levi (2015).

TUNAJIFUNZA NINI?
Kama watu tunaotafuta mafanikio, hatupaswi kuangalia udhaifu wa miili yetu. Japokuwa tuna udhaifu fulani katika viungo vyetu, bado Mungu ametupa akili ya kupambana na tukafanikiwa.

No comments:

Post a Comment