TTCL

EQUITY

Tuesday, January 26, 2016

Wanafunzi wagoma baada mwalimu mkuu kushushwa cheo

Wanafunzi wa shule ya sekondari Buruba katika manispaa ya Shinyanga, wamegoma kuingia darasani kuendelea na masomo kwa madai ya kupinga kushushwa cheo aliyekuwa mkuu wao wa shule, Alexander Yegera, kwa miaka 20 na kuwa mwalimu wa kawaida.
 
Wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari Busurwa, Uhuru, Mazinge, Buluba, Chamaguha, Kizumbi. 
 
Tukio hilo limetokea jana asubuhi baada ya wanafunzi hao kuandamana hadi kwa meneja wa shule hiyo, Joseph Mihangwa, katika jengo la Shirecu jirani na ofisi za mkuu wa mkoa Shinyanga, wakipinga uamuzi uliochukuliwa wa kushushwa cheo mkuu huo wa shule ambaye bado wanamuhitaji.
Wakizungumza mapema jana, baadhi ya wanafunzi hao, Geogre Boniface na Mariamu Salumu kwa niaba ya wenzao, walisema hawajaridhishwa na uamuzi wa bodi ya shule hiyo kwa kumshusha cheo mwalimu mkuu wao ambaye bado wanamhitaji kutokana na kusikiliza matatizo ya wanafunzi na kuyatatua kwa haraka.
“Hatutaingia madarasani mpaka tuhakikishe mwalimu wetu anarudishiwa cheo chake, hatumtaki mtu ambaye ameteuliwa kushika nafasi hiyo, John Ndama, sivyo inaweza kutokea vurugu na wengine kuhama shule hii,” alisema Boniface.
Hata hivyo, wanafunzi hao waliendelea na vurugu hizo na kusababisha jeshi la polisi kuingilia kati na kutuliza ghasia hizo na kuwaamuru wanafunzi hao warejee shuleni hali iliyofanikiwa, lakini waliendelea kugomea kuingia darasani hadi watakapotatuliwa tatizo lao.
Naye meneja wa shule hiyo, Joseph Mihangwa, aliyefika shuleni hapo muda mfupi, alizungumza na wanafunzi hao akiwa chini ya ulinzi mkali na kuwataka warejee madarasani huku kilio chao kikisikilizwa baada ya bodi ya shule kukaa.
Akizungumzia suala hilo, mwalimu anayepiganiwa na wanafunzi hao, Alexander Yegera, alisema Januari 20, mwaka huu, alipokea barua ya kushushwa cheo kwa madai taaluma yake ya uongozi imeshuka pamoja kutengeneza makundi ya walimu, hivyo kuridhia hali hiyo.

No comments:

Post a Comment