TTCL

EQUITY

Tuesday, January 12, 2016

Rais MAGUFULI amtembelea Sumaye, ahani msiba wa Leticia Nyerere

Rais JOHN MAGUFULI amemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu FREDERICK SUMAYE ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa MUHIMBILI jijini DAR ES SALAAM
 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Jumatatu Januari 11, 2016
 
Rais JOHN MAGUFULI amemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu FREDERICK SUMAYE ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa MUHIMBILI jijini DAR ES SALAAM, katika Taasisi ya Moyo ya JAKAYA KIKWETE.

Katika mazungumzo yao SUMAYE amemsifu Rais MAGUFULI kwa kuwajali watanzania bila kuangalia itikadi zao za vyama.

Katika hatua nyingine, Rais MAGUFULI amekwenda nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu JULIUS NYERERE kumpa pole Mama MARIA NYERERE kufuatia kifo cha LETICIA NYERERE aliyefariki dunia akiwa nchini MAREKANI.

LETICIA NYERERE alikuwa mbunge wa viti maalum katika bunge la 10 lililomalizika mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment