Afisa anayesimamia masuala ya haki za kibinaadamu
katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa ana ushahidi kwamba vikosi vya
usalama vya Burundi viliwabaka wanawake vilipokuwa vikitafuta nyumba za
wafuasi wa upinzani

Zeid
Ra'ad al Hussein amesema kuwa unyanyasaji huo ulitokea baada ya
shambulio la waasi katikati ya mwezi Disemba dhidi ya kambi tatu za
kijeshi.
''Ishara zote ikiwemo kuongezeka kwa mgogoro wa kikabila zinaonyesha ushahidi'',alisema katika taarifa.
Burundi ipo katika hali ya sintofahamu kutokana na Rais wa nchi hiyo
Pierre Nkurunzinza kujiongezea muda wa kuendelea kuongoza nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment