TTCL

EQUITY

Thursday, January 7, 2016

Serikali iwe makini na mipango miji

Utii wa sheria bila shuruti ni changamoto kubwa sana kwa watu wa rika zote hapa nchini, ndiyo maana matukio ya kuchomwa moto kwa vituo vya polisi, kupigwa kwa watu hadi kuuawa, mapigano baina ya wakulima na wafugaji vimerindima kila kona.
Kwa mujibu wa sheria ya mipango miji ya mwaka 1979 inakataza watu kufanya shughuli za kibinadamu, kujenga kwenye vyanzo vya maji ikiwemo mito na mabonde hadi umbali wa mita 60 ili kulinda vyanzo vya maji na kufanya mazingira yawe rafiki kwa binadamu.


Kwa kipindi chote serikali imekuwa ikifidia na kutoa misaada mbalimbali kwa watu wanaoishi mabondeni ambapo kwa upande wa Dar es salaam viwanja 1,007 vya Mabwepande vilitolewa kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko mwaka 2011 na baada ya mafuriko kwisha wananchi wengine waliamua kurudi katika maeneo yao ya awali na kuendelea na shughuli kama kawaida ambapo sasa hivi serikali imeamua kuwabomolea .
Kwa kutotii wito wa serikali pamoja na maafisa wa mipango miji pamoja na watu wa mazingira kutochukua nafasi zao mapema kumewafanya wananchi wengi nchini kujenga katika maeneo ya barabara,mito,maziwa,bahari,chemchem,pamoja na mabonde ambapo sasa hivi wananchi wengi zaidi ya 200,000 kwa Dar es salaam pekee kukosa makazi ya kuishi kwa kubomolewa nyumba zao.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadik ni kwamba watu wote watakaobomolewa nyumba zao kutolipwa hata shilingi tano na pia hakutakuwa na viwanja vya fidia .
Hii inaashiria kwamba lengo la serikali ni jema la kutaka kulinda wananchi na afya zao pia kulinda mazingira lakini serikali pia ililegalega katika kuhakikisha inasimamia sheria zake mapema kuliko kuwaaacha wananchi hadi leo wakiimarisha maeneo yao na kuanza oparesheni hii ambayo madhara yake ni makubwa sana kwa wananchi.
Mfano katika bonde la mto Msimbazi wananchi wameanza kujenga kuanzia miaka ya 1979 na serikali kupitia mashirika yake ya umeme na maji yamewawekea wananchi huduma zote na miji yao kutambulika kwa wakazi kupewa huduma zote za kiserikali na kushiriki kwenye sensa, kura na mengineyo na serikali kushiriki kuwasaidia kwenye maafa mbalimbali wakati wote huo serikali ilikuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi sahihi kuliko muda wote huo kuacha vizazi kwa vizazi kuzaliana na sasa kufukuzwa.
Ni vyema serikali ikatekeleza sheria zake inazozitunga kwa vitendo na kwa wakati bila kubagua masikini na matajiri ili kuhakikisha kunakuwa na mizania sawia katika upatikanaji wa haki kwa pande zote,pia maafisa miji na maafisa ardhi watoke maofisini wapime viwanja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya maeneo wanayotaka kununua na kujenga.

Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini (THRDC), wameyataka mashirika na taasisi za kusaidia jamii, makanisa na misikiti kuwasaidia watu wanaovunjiwa nyumba zao na kuachwa bila makazi.
 
Mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Onesmo Olengurumwa akizungumza na waandishi wa habari
 
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa taasisi hiyo Onesmo Ole Ngurumwa wakati akiongea na East Africa Radio juu ya zoezi la bomoa bomoa linaloendelea nchi nzima na kuongeza kuwa serikali ilifanya makosa kuacha watu wajenge maeneo hatarishi na yasiyoruhusiwa na hivyo wanawajibika kuwatafutia maeneo mbadala ya kuishi kabla ya kuwavunjia nyumba zao.
Ole Ngurumwa ametahadharisha kuwa watu laki mbili watakaoathirika na zoezi hilo watazalisha wezi na watu wasio na makazi na watoto wengi wa mitaani kitu ambacho ni hatari kwa jamii.
Aidha Onesmo Ole Ngurumwa amesema kuwa Tanzania ina eneo kubwa ambapo serikali ingeweza kuwajengea nyumba za gharama nafuu na kuwahamishia huko kabla ya kuwavunjia kama alivyofanya Rais wa kwanza wa Zanzibar mzee Abeid Karume.


Nyota wa filamu Wastara Juma
Aidha Nyota wa filamu Wastara Juma, akiwa moja ya mastaa wanaoguswa na zoezi la bomoa bomoa linaloendeshwa na serikali ambapo nyumba zake mbili zipo katika eneo lisiloruhusiwa, ametoa lawama nzito kwa niaba ya waathirika wengine wote katika zoezi hilo.
Wastara amesema, anatoa lawama kwa Serikali akiwa moja ya wananchi walioipigia kampeni kwa nguvu, zoezi hilo likimuacha na mzigo wa watu 28 wanaomtegemea bila makazi huku akiwa anahitaji matibabu ya pesa nyingi pia.

No comments:

Post a Comment