TTCL

EQUITY

Thursday, January 7, 2016

Prof. Ndalichako ahoji sababu za kubadili madaraja

Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Dk. Joyce Ndalichako amelipa siku saba Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kumpa maelezo ya kitaaluma ya kwa nini walibadilisha mifumo ya ufaulu.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Dk. Joyce Ndalichako amelipa siku saba Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kumpa maelezo ya kitaaluma ya kwa nini walibadilisha mifumo ya ufaulu.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam alipotembelea baraza hilo, Dk. Ndalichako amesema kuwa amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wadau wa elimu na wananchi juu ya mabadiliko ya mifumo ya ufaulu toka ule wa Divisheni mpaka wa GPA ambao wadau hawakushirikishwa wakati wa kufanya mabadiliko hayo, hivyo anautilia shaka kama una tija na kutaka maelezo ya kina ili kuutathmini kama unafaa ama la.
Akizungumzia Mfumo huo wa Wastani wa alama GPA, Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt.Charles Msonde amesema mfumo huo ulikubalika utumike katika kuanisha kiwango cha ufaulu wa wanafunzi baada ya NECTA kwa kushirikiana na wadau wengine wa elimu kwa kufuata maagizo ya waziri wa elimu wa wakati huo pamoja na watendaji wa juu wa wizara.
Aidha Prof. Ndalichako amewataka watendaji wa Baraza hilo kuhakikisha wanaangalia upya mfumo mzima wa ufundishaji katika shule ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa kuangalia zaidi uelewa wa wanafunzi wanao hitimu.
Kwa upande mwingine Waziri Ndalichako ametaka maelezo ya kutahiniwa wanafunzi wa kujitegemea kwa kutumia mitihani miwili ikiwa ni pamoja na mtihani wa upimaji endelevu ambao umekuwa ukifanyika wakati mmoja na mtihani wa kuhitimu vinginevyo wataifuta mitihani hiyo.
Profesa Ndalichako ametaka pia maelezo ya kwa nini watahiniwa wanatungiwa mitihani migumu, na kulitaka baraza hilo kufanya kazi na maamuzi yake ki uweledi zaidi pamoja na kuwashirikisha wadau wote katika sekta ya elimu ili kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini.

No comments:

Post a Comment