Taarifa kutoka nchini Ubelgiji zinasema kwamba, mchezaji wa kimataifa
wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo DR
Mbwana Samatta muda wowote anaweza kujiunga na klabu ya Genk
inayoshiriki ligi kuu nchini Ubelgiji (Belgian Pro League).
Kwa muda mrefu sana kulikuwa na harakati za Mbwana Samatta kujiunga
na vilabu vya Ulaya, klabu ya Genk ya Ubelgiji kwa asilimia nyingi ipo
kwenye dakika za mwisho kukamilisha deal la kumsajili Mbwana Samatta
kutoka TP Mazembe.
Genk ipo nafasi ya sita (6) kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini
Ubelgiji ikiwa imecheza michezo 20 na kufanikiwa kukusanya jumla ya
pointi 28 hadi sasa.
Moise Katumbi ambaye alikuwa anaonekana kama kikwazo yupo Ubelgiji na
jana alikuwa anafanya mazungumzo na timu ya Genk na kufikia makubaliano
ambapo na yeye pia amekubali kumruhusu Mbwana Samatta.
Dirisha dogo la usajili kwa vilabu vya Ulaya litakapofunguliwa mwezi January Samatta atatua Belgium kujiunga na klabu hiyo.
Samatta amebakiza mkataba wa miezi minne pekee kuendelea kusalia
kwenye klabu yake ya TP Mazembe ambayo msimu huu ameisaidia kutwaa kombe
la klabu bingwa Afrika.
Samatta akizungumza kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari kwenyepress conference tangu ajiunge na klabu ya Genk
Mara baada ya Mbwana Samatta kukamilisha taratibu zote za kujiunga na
klabu ya Genk, nyota huyo wa kwanza kutoka Bongo kwenda kucheza
professional soccer barani Ulaya aliongea mbele ya waandishi wa habari
akieleza anavyojisikia mara baada ya kukamilisha usajili wake wa
kujiunga na klabu hiyo.
Samatta amesema alikuwa anahisi anakuwa chizi kutokana na furaha
aliyokuwa nayo baada ya dili hilo kukamilika ambalo limeifanya ndoto
yake ya siku nyingi ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya kukamilika.
“Nilikuwa nahisi nakuwa chizi kutokana na furaha niliyokuwa nayo.
Ukiwa na ndoto halafu unaona ndoto yako inakuwa kweli, na kilichotokea
ni kama kuna giza mbele na unashindwa kuona hicho ndicho kilichotokea
kwangu”, alisema Samatta.
“Naiheshimu TP Mazembe, namuheshimu Rais wa Mazembe Moise Katumbi.
Sitaki kusababisha matatizo yoyote na wao kwasababu wamenichukua tangu
nikiwa mdogo na kunilea. Nimekulia Mazembe nikisubiri wakati muafaka
hadi klabu yangu ifikie makubaliano na klabu inayonihitaji”.
Samatta amesaini kandarasi ya miaka minne (4) kukitumikia kikosi cha
Genk ambapo anatarajia kuhudumu kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2020.
No comments:
Post a Comment