TTCL

EQUITY

Saturday, January 30, 2016

Elimu ya sheria Dar kuanza Januari 31

Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa sheria wanatarajia kutoa elimu ya sheria katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga alipokuwa akisisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo.

‘’Natoa wito kwa wananchi kuhudhuria maadhimisho ya siku ya sheria nchini yanayoashiria kuanza mwaka mpya wa shughuli za mahakama”Alisema Kattanga.

Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ya mwaka huu ni “huduma za haki kumlenga mwananchi:wajibu wa mahakama na wadau”

Ameongeza kuwa,miongoni mwa wadau watakaoshiriki katika kutoa elimu ya sheria ni pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Taasisi ya Sheria kwa Vitendo Tanzania (Law School), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA),Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Takukuru pamoja na Polisi.

Aidha Kattanga amesema kwamba wadau hao watatoa huduma za kisheria na kimahakama  kwahiyo wananchi wenye mashauri ya muda mrefu,malalamiko yoyote na mapendekezo ya uboreshaji wa utendaji kazi wa mahakama wafike na kuonana na waheshimiwa Majaji, Mahakimu,Wasajili na Watendaji wa Mahakama.

Maadhimisho hayo hufanyika nchini kila mwaka katika wiki ya kwanza ya mwezi wa pili ambapo kwa Jiji la Dar es salaam inatarajia kufanyika tarehe 31 Januari hadi Februari 3.

No comments:

Post a Comment