Ikiwa
ni siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabadiliko ya
Tabianchi wa Nchi Wanachama COP21 uliokuwa ukifanyika Paris, Ufaransa,
ambao ulimalizika kwa kupitisha mkataba mpya wa mabadiliko ya tabianchi
(Paris Agreement), wadau mbalimbali wamekutana kujadili matokeo ya
mkutano huo.
Mkutano
huo wa wadau umeandaliwa na ForumCC kwa kushirikiana na Rosa Luxemburg
Stiftung (RLS) kwa lengo la kuangalia mazidi na mapungufu ya mkataba huo
ambao umeweka historia mpya ya kuelekea juhudi za kupunguza ongezeko la
joto duniani, kukabiliana na kupunguza madhara ya mabadiliko ya
tabianchi.
Miongoni
mwa vipengele vya mkataba huo vilivyojadiliwa na wadau hao ni pamoja na
Kiwango cha nyuzi joto, Upunguzaji wa gesi Joto, Kukabiliana na
mabadiliko ya tabainchi, Uharibifu na upotevu, Fedha za mabadiliko ya
tabianchi, Mfumo wa taasisi na ushiriki wa serikali, waandishi wa habari
pamoja na asasi za kiraia kwenye kuleta mchango wa makubaliano ya
mkataba huo.
Picha ya pamoja ya Wadau hao.
Mwakilishi
wa ForumCC, Adam Athony akitoa mrejesho wa kilichojiri kwenye Mkutano
wa Mbadailiko ya Tabianchi COP21 uliofanyika Paris, Ufaransa
Mwakilishi
wa Rosa Luxemburg Stiftung (RLS) Afrika Mashariki, Musa Bulegeya
(katikati)akizungumza jambo wakati wa mkutano huo, kulia kwake ni Meneja
Miradi ForumCC Rebecca Muna, wakati kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya
ForumCC Yunista Kibona.
Mwandishi
wa habari na Mmiliki wa mtandao wa Tabianchi, Dotto Kahindi akitoa
mrejesho wa yale aliyojifunza kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi
COP21, Uliofanyika Paris, Ufaransa.
Washiriki wakifuatilia mkutano huo
Mwakilishi
wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ladslaus Kyaruzi akielezea namna
Tanzania ilivyoshiriki kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi
COP21.
No comments:
Post a Comment