TTCL

EQUITY

Thursday, December 24, 2015

Umuhimu wa wafanyakazi wenye ujuzi ndani ya sekta ya utalii

20151207_104824
Meneja Mkazi wa kampuni ya JovagoTanzania, Bw. Andrea Guzzoni.

 “Maendeleo ndani ya sekta ya Utalii hayawezi kufikia kiwango nzuri iwapo hakutakuwa na wafanyakazi wenye ujuzi wa kutosha”
Kukua kwa sekta ya utalii kunategemea hudumu za ukarimu kwa kiasi kikubwa. Huduma hizi zinapaswa kufanywa na wajuzi waliobobea ndani ya sekta  ili kuweza kuwaridhisha wageni na kuleta maendeleo katika soko hili la utalii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Mkazi wa kampuni ya JovagoTanzania, Bw. Andrea Guzzoni alifafanua kuwa, ukarimu  na ujuzi wa kutosha kwa wahudumu wa mahotelini na sekta malimbali za utalii ni jambo muhimu kwa kuwa litaongeza pato la taifa kutokana na ongezeko la wageni watao hitaji huduma hizo bora na zenye viwango .
Watanzania inabidi tufahamu kuwa kila mtu akiwa nje ya  eneo la nyumbani kwake atahitaji apate huduma kama ya nyumbani kwake au na zaidi, hivyo tuzingatie matuzi ya lugha nzuri, na huduma za viwango vinavyotakiwa”.
Aliongezea kwa kufafanua kuwa, “Hata hivyo bado hoteli nyingi zinaajiri wafanyakai wasio na elimu ya kutosha, wafanyakazi ndani ya sekta hii wanatakiwa kujua lugha zaidi ya mbili ikiwemo lugha za kimataifa, lakini kwa Tanzania wahudumu wengi hawafamu lugha hii ya  kigeni na kumpa shida mtalii wa nje
 Tutambue kuwa huduma ndani ya sekta ya utalii au mahotelini haziwezi  kuwaridhisha watalii kwa njia za mashine bali watu wenyewe. Hivyo Wafanyakazi wana nafasi kubwa katika kukuza sekta hii ukiringanisha na sekta nyingine zinazoweza kutendeka bila ya nguvu kazi za watu.
Kwa upande wake, Bw. Richard Rugumbana wa Tourism Confederation of Tanzania (TCT) alifafanua kuwa “Serikali pamoja na sekta binafsi tujitahidi kutilia mkazo kuongeza mafunzo ya ziada ya taaluma ya utalii, “Ni vizuri tukajifunza mafunzo ya ndani na nje ya nchi yaliyobobea,  pia tuweke  utaratibu wa kuwaongezea ujuzi wafanyakazi tuliowaajiri na kuwapa vipaumbele  kwa wafanyakazi wenye elimu ya juu kama kuwapa vipato vinavyoendana na elimu yao. ”

No comments:

Post a Comment