WASANII Wakongwe katika tasnia ya filamu Swahilihood leo tarehe 16Th
December, 2015 katika ukumbi wa Idara ya Habari ya Maelezo wametoa tamko
lao kuhusu kumtaka Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon
Mwakifwamba kugombea nafasi hiyo ambayo alitangaza kutoshiriki kugombea
nafasi hiyo kwa kipindi kijacho uchaguzi huo mwezi huu 2015.
Wasanii wakongwe wakitoa tamko lao kuhusu Rais Mwakifwamba |
Baada ya salamu hizo kwenu tumekuja hapa kwa tukiwa na ya kuwaeleza
wanahabari sote mnatujua kwa kutuona au kuona kazi zetu kupitia katika
filamu hata vyombo vyenu, kwanza tunaanza kwa kumpongeza Rais wetu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa
kuwa Rais na utendaji wake sote tumeona na kutupa faraja kubwa sana
kama Watanzania.
Pili pongezi zetu ziende kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
michezo Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Moses Nnauye kwa
kuchaguliwa kuwa Waziri wetu na moja kwa moja tunaona Nuru kwetu ikija
baada ya kuwa katika kipindi chenye changamoto nyingi tukiwa kama
wasanii wakongwe hapa nchini Tanzania.
Baada ya utangulizi huu mzito wenye tija sasa tuseme kilichotufanya
tuone haja ya kuongea na nyinyi wanahabari wadau wetu ambao tunaamini
kabisa sauti yenu inafika mbali zaidi baada kuidaka na kuirusha katika
vyombo vyenu yaani magazeti, redio, Runinga na mitandao ya kijamii kwa
ujumla wake, sote tu mashahidi kuwepo kwa chombo chetu wasanii ambalo ni
shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF).
Shirikisho hili lina uongozi wake mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi kwa
masikitiko makubwa Rais wa Shirikisho hili na mtendaji mahiri Bwana
Simon Mwakifwamba alitangaza kutogombea tena nafasi ya Urais lakini sisi
kama ndio Wasanii wakongwe katika tasnia hii tunapinga uamuzi wake na
kumuomba abadilishe fikra hizo na agombee tena kwani tumeona Nuru
imekaribia kwetu, baada kwa muda mrefu kukosa kitu kinachotuweka pamoja.
Waswahili usema mji usio na Wazee na kusikilizwa mji huo ukosa hekima
na Busara na hatimaye uzaa madhara na kuleta uharibifu, kwetu tunaona
hilo hatutoliruhusu litokee kwani mmekuwa mashahidi pale baadhi ya
wasanii wakiongea vitu vya hovyo kabisa tena kwa migongo yetu bila
kutushirikisha tunahitaji kiongozi mwenye upendo na kutuunganisha si wa
kutugawaga, naye ni Simon Mwakifwamba.
Tumeshuhudia miradi mingi ambayo imehasisiwa chini yake na
haijakamilika vema aingie tena kumalizia kazi aliyoianza, kuna TAFF
TRUST FUND, pia TAFF CREATIVE LTD miradi hiyo yote inahitaji umakini
mkubwa katika kuhakikisha inasimama na kutuokoa wasanii bila kusahau
Sera ya filamu ambayo inasubiri kupitishwa na Serikali inahitaji mtu
makini na mfuatiliaji kama Mwakifwamba.
TAFF TRUST FUND ni mfuko wa wasanii wa filamu ambao utatusaidia sana
katika utendaji wetu ni kitu muhimu sana hakuna mtu aliyefikiria kuhusu
wasanii wa filamu kuwa na mfuko wao, TAFF CREATIVE LTD huyu ni mkombozi
kwetu kwani kazi zetu zimekuwa na changamoto kukosa soko la uhakika
kampuni hiyo itasaidia kubororesha maslahi katika tasnia ya filamu
Tanzania.
Tuna mengi lakini kwa leo nafikiri hayo yanatosha kwa kifupi pia
nimeongozana na wenzangu wana yao ya kuongea tukimuomba Mwakifwamba
abadilishe mawazo yake na kuendelea nasi tukiwa kama wazee wake washauri
tunahitaji mtu ambaye atakwenda na kasi ya Rais wetu Dkt. Magufuli .
Asanteni kwa kunisikiliza
Mratibu
WASANII WAKONGWE KATIKA TASNIA YA FILAMU
No comments:
Post a Comment