TTCL

EQUITY

Friday, December 25, 2015

Rais MAGUFULI ashiriki katika misa ya KRISMAS

Rais Dokta JOHN MAGUFULI amewaongoza wananchi katika misa takatifu ya Krismas kwa kuwataka wananchi kupendana, kuwa na umoja
 
Rais Dokta JOHN MAGUFULI 
 
Rais Dokta JOHN MAGUFULI amewaongoza wananchi katika misa takatifu ya Krismas kwa kuwataka wananchi kupendana, kuwa na umoja na kumtanguliza mungu katika maisha.

Akizungumza katika misa iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro OYSTERBAY Jijini DSM, Rais MAGUFULI amewahimiza wananchi kuendelea kuliombea taifa ili kuweza kutekeleza azma na malengo yaliyowekwa.

Rais MAGUFULI pia ameutumia muda huo kuwataka watanzania kuendelea kuwa na mshikamno na upendo, bila kusahau kufanya kazi ili taifa liweze kusonga mbele.

Naye Padre JOSEPH MOSHA ambaye aliongoza ibada takatifu ya krismas katika kanisa hilo, amesema kuzaliwa kwa YESU KRISTO ni ishara tosha kwa mwanadamu kuwa amezaliwa upya

No comments:

Post a Comment