TTCL

EQUITY

Friday, December 18, 2015

Kwa nini Umuache Mumeo Kisa Umemfumania?


 

Habari zenu wasomaji wa safu hii, bila shaka ni wazima na mnaendelea vema na kazi za kulijenga taifa letu.
Binafsi namshukuru Mungu, hii leo nimekuja na mada mpya ya kukupa ujasiri ili usiikimbie nyumba yako kwa sababu umemfumania mumeo.
Wanawake wengi wamekuwa na tabia ya kuwafuma waume zao na kwa hasira kuamua kuwaacha na kwenda nyumbani wakishakaa huko wanaanza kutamani kurudi hivi kwa nini wanafanya makosa kama hayo!
Nimeandika mada hii kutokana na ujumbe niliotumiwa na msomaji wangu ambao ulikuwa ukisomeka hivi;
“Mama mimi ni msomaji wako mzuri, nashukuru kwa kutupa elimu ya mapenzi inayosababisha tukapata ujasiri wa kuendelea na ndoa ambayo bila kuwa mvumilivu unaweza kujikuta unasema sitaki tena ndoa, mama wiki mbili zilizopita nilimfumania mume wangu akiwa na mwanamke mwingine ambaye huko nyuma nilikuwa nikimuuliza ni nani ananiambia anafanya naye kazi ni rafiki wa kawaida.
Nilipomfuma mume wangu niliamua kuondoka nyumbani kwa maana ya kuachana naye ingawa aliniomba msamaha lakini niliumia kuona siku zote alikuwa akinidanganya.
Kwa sasa nipo njia panda kwani nampenda mume wangu na tayari nimepoteza vitu vingi ambavyo nahisi maisha yangu ndiyo yapo hapo kutokana na ugomvi wetu, pia tuna watoto watatu nifanyeje ili kulimaliza hili?” anauliza mama Pili wa Kimara.

Hili liwe fundisho kwa akina mama wote
Si kama nawatetea wanaume na nataka wawe na tabia ya usaliti kupitia makala haya lakini nataka niwape fundisho akina mama kwa sababu wanaume wengi ndiyo tabia zao, kwa nini uache nyumba yako, watoto wako na malengo yako yote kwa sababu tu ya mwanamke wa nje ambaye umemfuma siku moja, eti akuharibie maisha yako?

Jikaze jifunge mkanda
Mwanamke umeumbwa kuwa jasiri hasa kutokana na mambo unayoyapitia nakusihi ukishamfuma mume wako usikurupuke kuondoka nyumbani kama vipi aondoke yeye mkosaji si wewe ambaye mwisho wa siku unamuachia nyumba mtu ambaye hajui hata mlianzia wapi mpaka mmefikia hapo, pia kumbuka kuwa utakuwa ukiwatesa watoto wako.

Mpe nafasi nyingine
Mume akikuomba msamaha msikilize na mpe masharti kwani wakati huo mume mwenye makosa ndiyo humpa raha mke ambaye si mkosaji kwa maana ya kumbembeleza, hebu tumia nafasi hiyo kumrejesha mumeo na kama kuna makosa ulikuwa ukiyafanya kwake yaweke sawa maana huenda kuna sehemu ulikosea ndipo akaamua kuchepuka nje na kumbuka ndoa inahitaji uvumilivu, kumkimbia mume siyo suluhisho.

No comments:

Post a Comment