TTCL

EQUITY

Saturday, December 19, 2015

Kona ya Kitime: Oya mwana usiringie uzuri, ringia bahati

andy-today 
Inakuwa nene masela wangu? Kipande hii ni mzuksi kichizi arifu. Kama vipi welikamu kwa sana kwa fasi ya hapa jamvini tukisanue mazee ama nini! Basi sawa.
Wanangu kuna ishu zingine hazihitaji mtu kuwa machi noo kozi kuna pipo ni mamasta maindi ileile na ukileta za kujua sana dheni watu wanakupiga chabo dheni wanakuchora tu si unajua zile? Kuna wale makaksi wa ukwehe ambao mara nyingi siyo wachangiaji wa mamada kiivo bati wana madini ile mbaya kwa kichwani! Ebana kitu cha holidei ya uhuu vepe? Mambo ya foto kanga na ekotite yalikuwa mpango mzima? Barida!
Basi bana huku na huku selaa wangu akamingo na chiki mmoko mkare aibu kiaje sasa mazee. Yaani usipimie kabisa kwa jentromani wa ukwehe achana na wale watoto mayai lazima uzime fegi kachala wangu.
Siyo siri wanangu mtoto ni sumu ile mbaya sema tu laifu lake huko nyuma lilikuwa la kukurukakara za hapa na pale wanangu wenyewe kwenye mambo yaleee ya kubadili mameni kama chizi f’lani hivi freshi.
Laifu limemuvu fasta na huwezi kubilivu si ndo msimu wa kitu cha holidei? Masela hii siyo taimu ya kumbwela ni mwendo wa maandalizi ya kufa mtu ili wanangu wasiaibike.
Unaambiwa jamaa yangu kazama ofisini kwa shori hapo dauni tauni Bongo tambarare kupata sevisi f’lani si ndo kachaa kadata na mtoto? Akaona isiwe kitu, baada ya kitambo f’lani hivi mwana akatangaza kuweka kitu na boksi ndani.
Sasa bana unajua ukitaka kugonga bata la holidei usimchunguze sana kozi hutalila kwa raha au hutalila kabisa. Basi bana, kabla ya kumweka kwa skani akaona amwekee spai wa kumchunguza kama ametulia au ndo kama hivo magumashi?
Yule msela aliyepandikizwa na mwana si ndo akaanza mbishe za kumfukuzia shori? Kama nilivyokuteli bifoo kwamba tabia ni kama rangi kuifuta ina kosti zake. Jamaa kamuimbisha shori hadi wakakubaliana wakafanye yao kwa hoteli!
Da! Noma sana wanangu! Shori amefika kwa mapokezi kakaribishwa freshi na bashasha za kumwaga kisha akapewa funguo za rumu.
Mazee wakati shori anamsikilizia jamaa akiwa amejimwaga kwenye peji ndani ya suti ya kuzaliwa, ghafla bin vuu mlango ukagongwa…kwenda kufungua shori hakuamini macho yake kukutana feisi kwa feisi na mchumba’ke orijino kumbe alikuwa amechezewa maindi tu.
Mnanyaka masela unajua kwenye hili laifu siyo ishu kuringia uzuri na kushindwa kujikontroo. Ni beta mazee mtu ukaringia bahati na siyo kitu cha sura na umbo bomba.
Ona sasa, pamoja na ukare wa shori bati kitu cha uchumba mwisho wa reli na laifu limestaki.

No comments:

Post a Comment