TTCL

EQUITY

Friday, December 18, 2015

Athari za upungufu wa damu kwa mama mjamzito

 
Mjamzito anakuwa na hatari kubwa ya kupoteza uhai wake pindi ajifunguapo ikiwa ana upungufu wa damu mwilini kwa sababu zoezi zima la kujifungua linahitaji damu ya kutosha, akipoteza damu nyingi ni hatari kwake kuishiwa damu mwilini.
Upungufu wa damu kwa mama humwathiri pia mtoto tumboni na kuzaliwa mwenye afya dhoofu aliye na uzito mdogo.
Upungufu wa damu husababisha mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake (njiti), mtoto kuwa na upungufu wa damu, kuzaliwa akiwa amechoka (fetal distress), ukuaji wake unadumaa na kusababisha maendeleo duni ya kiakili.
Wajawazito wenye hatari zaidi wa kuwa na upungufu wa damu mwilini ni wale wenye kushika mimba ya zaidi ya mtoto mmoja (mapacha), wenye mimba za utotoni na walio na matatizo ya upungufu wa damu kabla ya kushika mimba.
Pia wenye kushika mimba kwa haraka baada ya kujifungua mtoto mwingine (bila kupisha miezi mingi), wanaokula lishe isijitosheleza madini ya chuma.

Tiba
Upungufu wa damu unaweza tibika kwa haraka na kuokoa maisha ya mama na mtoto, kinachotakiwa mama anahitaji kupima kiasi cha damu kila ahudhuriapo kliniki na anaweza kuongeza damu kwa kutumia vidonge vya madini ya chuma kwa miligram 2-4.8 kwa siku.
Mjamzito anaweza kuongeza damu kwa kutumia vidonge (supplements) za Folic Acid, zinasaidia kuongeza kiasi cha damu kwa haraka.
Ushauri unatolewa wa kutumia matunda ya beetroot ambayo huchemshwa na kutengeneza juisi , unaweza ukasaga ukanywa au ukapikia kwenye chakula zinapatikana masokoni, kwa mfano Dar es Salaam kwenye Soko la Kisutu au Kariakoo.
Unaweza kuongeza damu kwa kula matunda kwa wingi, tafuna au kunywa juisi ya nyanya, rosella glasi 2-3 kwa siku na kula mboga za majani kama spinachi, mchicha, brocoli au matembele kwa wingi.
Kula dagaa au kunywa supu ya maharage kwa wingi, kula nyama, kuku na samaki, kunywa maziwa, cheese na kula mayai.

USHAURI
Zingatia kupima kiasi cha damu mara kwa mara uendapo kliniki, ni hatari kupungukiwa na damu ukiwa na ujauzito lakini hata kwa mtu ambaye hana mimba, ni hatari pia kwake akiwa hana damu ya kutosha.

No comments:

Post a Comment