Kama uliangalia mechi vizuri kati ya TP Mazembe na USM Alger ni
kwamba pale Mbwana Samatta alipofunga penati, alikimbilia kwa mashabiki
na kuchukua bendera ya Tanzania.
Sasa story kuhusu ile
bendera ni kwamba ilitengenezwa na watanzania wanaoishi Lubumbashi baada
ya kukosa bendera ya Tanzania walivyotaka kwenda uwanjani.
Walichokifanya ni kutafuta vitamba vya blue, nyeusi na njano
wakaunganisha kama unavyoona kwenye picha ili kutengenezea bendera ya
Tanzania. Tatizo likaja pale kupata rangi ya blue ili kukamilisha bendera
ya Tanzania.
hivyo ikawalazimu kuchukua kitambaa cha Zambarau kama unavyoona
hapo na kujiridhisha kwamba hiyo ni bendera ya Tanzania. Waliingia nayo
uwanjani na bahati nzuri wakapata kiti cha mbele na Mbwana Samatta
akaenda kuichukua ile bendera bila kujua.
Mwisho wa siku ilikua ni katika harakati za kuonyesha uzalendo wa
Tanzania na kuwapa support watanzania Thomas Ulimwengu na Mbwana
Samattha walikua wanacheza mechi ile.
No comments:
Post a Comment