TTCL

EQUITY

Wednesday, November 25, 2015

FIFA yaboresha ushiriki wa wanawake katika soka

Chama cha Soka la Wanawake nchini TWFA kimesema mpango wa kuhamasisha wanawake kujihusisha na soka ulioandaliwa na FIFA unaotarajiwa kuzinduliwa rasmi Novemba 29 mwaka huu jijini Dar es salaam utasaidia kuweza kukuza soka kwa wanawake hapa nchini.
Mwenyekiti wa TWFA Amina Karuma, amesema lengo la programu hiyo ni kuhakikisha wanawake wote na wa umri wote wanashiriki kwa namna moja au nyingine kwenye mpira wa miguu wa wanawake.
Karuma amesema, japo programu hiyo inahusisha wanawake pekeyake lakini wanaume wanatakiwa kujitokeza ili kuweza kutoa sapoti japo watakaocheza ni wanawake lakini wanahitaji sapoti ili kuweza kupata ushauri kutoka kwa wanaume ambo Soka lao lipo juu kwa sasa hapa nchini.
Kwa upande wake Balozi wa Soka la wanawake wa FIFA ambaye pia ni mlinda mlango wa timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars Fatma Omary amesema, wazazi wanatakiwa kuwaruhusu watoto wa kike ili kuweza kushiriki katika soka la wanawake na kuweza kuongeza vipaji hapa nchini.
Programu hiyo iliyoandaliwa na FIFA ilizinduliwa rasmi Julai tano mwaka huu Mkoani Geita ambapo inawakilishwa na mabalozi kutoka timu ya taifa ya Tanzania Twiga Stars ambao ni kocha msaidizi Edna Lema, aliyekuwa mshambuliaji wa Twiga Stars Esther Chaburuma 'Lunyamila', Mlinda Mlango Fatma Omary na Nahodha Sophia Mwasikili.

No comments:

Post a Comment