TTCL

EQUITY

Friday, June 19, 2015

Kadinda: Wema anawakati mgumu, na changamoto kubwa kwenye siasi


Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amesema anaamini kuwa muigizaji huyo anaweza kuwa kiongozi mzuri japo changamoto inayomkabili ni kubadilisha mawazo ya watu juu yake hasa kutokana na maisha yake ya ustaa na mapenzi.

Martin ameiambia Bongo5 kuwa kinachotakiwa sasa ni kuwabadili watu waanze kumchukulia kama mwanamke anayeweza kuwa kiongozi. 

“Watu wengi wametokea kumsupport kwa sababu walikuwa wanamsikia baba yake akimtaka aingie kwenye siasa, na wengine walikuwa wanamtaka Wema aingie kwenye siasa,”amesema Martin.


“Lakini ana kazi kubwa ya kuweza kubadilisha watu jinsi wanavyomchukulia. Kwahiyo anachukulia positive kwa sababu watu aliokuwa nao wameweza kumsupport. Lakini kabla hatujafika huko sasa tutamuona kama kiongozi sioo kama msichana wa bongo movie. Tumuamini Wema kama anaweza kuonyesha tu nia hata asipopata tukumbuke kuonyesha nia tu ni kupata, kwa sababu ana ndoto kubwa sana anataka kuzifanya,” ameongeza.

Hivi karibuni Wema alitangaza nia ya kuwania ubunge wa viti maalum kwa tiketi cha chama cha mapinduzi mkoani Singida.

No comments:

Post a Comment