TTCL

EQUITY

Tuesday, March 10, 2015

GEPF YATOA SEMINA KWA MAAFISA UTUMISHI KANDA YA ZIWA,MKUU WA MKOA AWATAKA KUWAPA KIPAUMBELE WATU WENYE MAKUNDI MAALUMU.

 MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULUNGO AKITOA HOTUBA KATIKA SEMINA HIYO YA MAAFISA UTUMISHI.

Mifuko ya hifadhi ya jamii nchini imetakiwa kuwapa kipaumbele watu wenyemahitaji maalum wakiwemo watu wenye ulemavu wa ngozi {albino} ili kuwainua kiuchumi katika shughuli zao.

Mwito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulungo wakati akifungua semina ya siku moja kwa mameneja rasilimali watu iliyoandaliwa na mfumo wa pensheni wa GEPF.

Mulungo amesema kuwa watu wenye mahitaji maalum wanashindwa kufikiwa kwa wakati na kupewa mikopo huku wengi wao wakiishi maisha duni na wengine kukimbia makazi yao kwa hofu ya kuuwawa.

Ameongeza kuwa ikiwa mifuko ya jamii itaweza kuwasaidia mikopo na kujiwekea akiba watatoka katika hali duni na kuwa na maisha salama kwao na familia zao.

Awali alimkaribisha mkuu wa mkoa kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa GEPF meneja masoko wa mfuko huo Alyoce Ntukamazina amesema kuwa mpaka sasa mfuko wa GEPF una wanachama wapatao elfu 50 ambao michango yao ya hiari imefikia shilingi bilioni 6.

Semina hiyo iliyojumuisha maafisa utumishi kutoka mashirika na halmashauri tofauti za kanda ya ziwa imelenga kutoa elimu kwa ili waweze kutoa ushauri mzuri kwa waajiliwa wapya.

MATUKIO KATIKA PICHA:

 MAAFISA TOKA GEPF WAKIWA KATIKA MEZA YA MAPOKEZI
KATIKA SEMINA HIYO.

 WAGENI WAKIWA WANAINGIA KATIKA UKUMBI KWA AJILI YA SEMINA.

 BAADHI YA MAAFISA UTUMISHI WAKIWA KATIKA UKUMBI
WAKISHIBISHWA MAMBO MAZURI TOKA GEPF.

 MAAFISA UTUMISHI WAKIBADILISHANA MAWAZO 

 SEMINA IKIENDELEA HAPA MAAFISA UTUMISHI WAKIJADILI JAMBO

 MENEJA MASOKO WA GEPF BWANA ALOYCE NTUKAMAZINA AKITOA MAELEZO KUHUSU MFUKO WA GEPF KWA MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESSA MULUNGO(KULIA)

 MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULUNGO AKITOA HOTUBA KATIKA SEMINA HIYO.

 MAAFISA WA GEPF WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MKUU WA MKOA HAYUPO PICHANI,

 MAAFISA UTUMISHI WAKIENDELEA KUMSIKILIZA MKUU WA MKOA MAGESSA MULUNGO HAYUPO PICHANI.

 AFISA MASOKO WA GEPF MWANZA BWANA JOSEPHAT NCHAMA AMBAYE NDIYE ALIYEKUWA MRATIBU WA SEMINA AKIENDELEA NA URATIBU KATIKA UKUMBI WA SEMINA.

 BAADA YA SEMINA WASHIRIKI WALIPATA MUDA WA KUPIGA PICHA YA PAMOJA NA MKUU WA MKOA WA MWANZA NA MAAFISA WA GEPF.

No comments:

Post a Comment