Itatokea mara chache ambapo utataka kuangalia TV kwenye kompyuta au simu. Kuna kipindi uko mbali na tv yako, iwe hotelini au ugenini na una kompyuta karibu. Pengine upo nyumbani na tv inatumika na mwanafamilia mwingine na ungependa kuangalia chaneli tofauti. Kuna uwezekano ukatumia kompyuta au simu yako kuangalia tv kwenye intaneti.
Jambo linalokuja akilini haraka sana ni kwamba intaneti ina gharama sana kwa matumizi haya. Zipo ofa za intaneti pekee na za usiku ambazo zitakupa uhuru wa kuangalia kwa mfano, mpira au hata muvi ambazo hazichukui ‘MB’ nyingi. Kuna njia tano tumekuwekea hapa kuangalia unachotaka mtandaoini.
Fungua Tovuti za Chaneli husika (hasa za habari)
Hizi ni rahisi kupata na ni salama zaidi. Tayari hapa nchini kwetu Tanzania kuna chaneli kadhaa za TV ambazo unaweza kuangalia mtandaoni kama
Pia, huko ughaibuni napo kuna utitiri wa chaneli za bure, iwapo tu ukajua tovuti yake na jinsi ya kuzifungua ukiwa nje ya mipaka yake ya kuoneshwa, kama
Ingia kwenye tovuti zinazokusanya chaneli za bure mahali pamoja
Angalia tv bure kwenye kompyuta yako kirahisi kwa kuchagua chaneli kwa na nchi au maslahi yako kwenye tovuti hizi ambazo zinakusanya liniki kwa chaneli zinazotangazwa bure kupitia intaneti:
Tovuti zinazoonesha Michezo (hasa soka)
Kuna tovuti kadhaa ukifanya ka-uchunguzi kidogo ambazo zinakusanya linki za tovuti za kuangalia mpira bure.
Ubora wa matangazo yanayopatikana kupitia linki nyingi siyo nzuri sana ila zinaangalika. Suala la msingi kuzingatia ni kwamba si rahisi kuangalia mpira kwa njia hii. Ukiwa mjanja, ukijaribu linki kadhaa na kupambana na matangazo utapata kuangalia mpira. Usifuatilie matangazo au kushusha kitu chochote kitachojitokeza, unaweza kupata virusi.
Matangazo ya papo kwa hapo kwenye Youtube na Tovuti nyingine.
Kuna vitu kama matangazo ya droo za FA, maonesho ya Apple, Samsung na mazungumzo ya watu flani ya teknolojia ambayo yanatangazwa kwenye intaneti tu.
Muvi mtandaoini.
Mdau mmoja, Maftah ametupatia tovuti ya kuangalia muvi bila kushusha kama unapenda kufanya kama hivyo au hata kushusha bila torrent – g2g . Utapata kuona muvi mpya na ‘episode’ mpya za ‘series’ zinazoangaliwa zaidi sasa.
Hitimisho
Ni jambo la kufurahisha kuweza kuangalia tv ukiwa mbali na tv au inatumiwa na mtu mwingine au kwa sababu nyinginezo. Ni dhahiri kwamba kuna changamoto kadha wa kadha ukitaka kuangalia tv kwenye intaneti.
Mtangazo, virusi na programu zinazofanya vivyo-sivyo (malware) huelea sana katika tovuti kama hizi. Si rahisi na inahitaji uvumilivu. Tovuti nyingi zitaacha kufanya kazi kwani si rasmi (za kuibia ibia, hamna kitu cha bure) na itakubidi ujiongeze mara kwa mara. Watoa huduma kama DSTV wanatoa app zao spesheli kwa ajili ya kukuwezesha kuangalia chaneli zako kadhaa kama za michezo kwenye simu au tableti yako.
No comments:
Post a Comment