Tukio limetokea jana Februari 24,2015 saa sita mchana katika eneo la Ilula wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa polisi walipofika eneo hilo watu waliokuwa eneo hilo walianza kukimbia kuhofia kukamatwa ndipo polisi mmoja akamchota mtama mwanamke mmoja aliyekuwa anakimbia,akaanguka na kufariki dunia hapo hapo.
Kufuatia kifo hicho, wananchi walihamasishana na kuanza kupambana na askari hao huku wakiwa wamebeba silaha za jadi ikiwemo fimbo na mawe,wakazuia magari yaendayo mikoani,kuchoma matairi barabarani huku polisi nao wakirusha mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi hao.
Inaelezwa kuwa wananchi hao mbali na kuharibu mali mbalimbali za polisi ikiwemo kuchoma moto magari matatu ya polisi kituo Ilula na vitu vingine vingi.
Mwakilishi wa Malunde1 blog mkoani Iringa Yonna Mgaya anayefanya kazi Radio Furaha ya Iringa amezungumza na kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Pudensiana Protas ambapo kamanda huyo wa polisi amesema polisi walipata taarifa kuwa kuna uuzaji wa pombe za kienyeji ikiwemo pombe haramu aina ya gongo na walipofika pale watu wakaanza kukimbia hovyo.
Kamanda huyo wa polisi amesema wakati wananchi wakikimbia ovyo ndipo huyo mwanamke akateleza na kuanguka akafariki dunia.
Kamanda Protas mesema polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo na jina la mwanamke aliyefariki halijafahamika na kwamba watatoa taarifa rasmi juu ya tukio hapo baadaye.
No comments:
Post a Comment