TTCL

EQUITY

Sunday, February 15, 2015

HIZI HAPA SHULE 10 BORA KWA UFAULU,10 ZA MWISHO NA WANAFUNZI 10 BORA ZAIDI MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2014

Akitangaza matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2014 leo jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt Charles Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 89,845 sawa na asilimia 66.61 wakati wavulana ni 106,960.



Akizitaja shule kumi bora kwa ufaulu, Dkt Msonde amesema shule hizo ni;
Kaizirege mkoa wa Kagera Mwanza Alliance mkoa wa Mwanza Marian Boys mkoa wa Pwani St. Francis Girls mkoa wa Mbeya Abbey mkoa wa Mtwara Feza Girls mkoa wa Dar es salaam Bethel sabs Girls mkoa wa Iringa Marian Girls mkoa wa Pwani
Feza Boys mkoa wa Dar es salaam.


Shule 10 za mwisho


Manolo mkoa wa Tanga, Chokocho mkoa wa Pemba, Kwalugulu mkoa wa Tanga
Relini mkoa wa Dar es salaam, Mashindei mkoa wa Tanga, Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma, Vudee mkoa wa Kilimanjaro, Mnazi mkoa wa Tanga
Ruhembe mkoa wa Morogoro, Magoma mkoa wa Tanga.



Dkt Msonde pia ametaja watahiniwa 10 waliofanya vizuri kuwa ni

Nyakaho Marungu kutoka Baobab Pwani
Elton Sadock Jacob kutoka Feza Boys Dar es salaam
Samwel M Adam kutoka Marian Boys Pwani
Fainess John Mwakisimba kutoka kutoka St Francis Girls Mbeya
Mugisha Reynold Lukambuzi kutoka Bendel Memorial Kilimanjaro
Paul W Jijimya kutoka Marian Boys Pwani

Angel Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya
Atuganile Cairo Jimmy kutoka Canossa
Jenifa Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya
Mahmoud Dadi Bakili kutoka Feza Boys.

No comments:

Post a Comment