TTCL

EQUITY

Monday, December 8, 2014

Zitto aitibua chadema

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, anachukizwa na kitendo cha Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) la kuweka sharti la kurejesha kundini.

Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote za uongozi mapema mwaka huu, kwa sasa yuko mahakamani akitetea uwanachama wake, baada ya viongozi wenzake wakuu kutishia kutaka kumfukuza.

Habari kutoka ndani ya Chadema zinasema, karibu viongozi wote wa juu wa chama hicho, akiwamo Dk. Willibrod Slaa, wameonyesha nia ya kumsamehe Zitto ili arejee kundini, lakini tatizo lilikuja pale mwanasiasa huyo alipoweka sharti.

Inadaiwa kuwa Mbowe ameweka msimamo mkali baada ya Zitto kutoa kauli inayoonyesha kuwa anataka kuwekwa sharti la yeye kurejea ndani ya chama.

“Kulikuwa hakuna tatizo Zitto kusamehewa na kurejea ndani ya chama. Lakini kauli yake kuwa anaweka sharti la kutaka kusamehewa, ndilo limeonekana kumkera mwenyekiti,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama ambaye hakupenda kutajwa.

Amesema baada ya Kamati ya Bunge ya PAC inayoongozwa na Zitto kufanya kazi kubwa ya kuchambua ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kisha kuwasilisha mapendekezo yake bungeni, baadhi ya viongozi wa Chadema akiwamo Mbowe na Dk. Slaa walionekana kuwa wako tayari kusamehe yaliyopita, lakini kitendo cha Zitto kuweka sharti kimewaudhi baadhi yao na kumuona kama mtu anayetaka kuabudiwa.

Mapema wiki iliyopita, Zitto alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema, "hajui kosa" lake na kuweka masharti kwamba pale atakapoambiwa kosa lake yuko tayari kuomba radhi na kurejea Chadema.

No comments:

Post a Comment