TTCL

EQUITY

Saturday, December 6, 2014

Tanzia: KOCHA ABDALLAH 'KING' KIBADEN AMEFARIKI DUNIA, SOMA HABARI KAMILI

Abdallah Kibaden aliwahi kuwa kocha wa Simba, Kagera Sugar na Ashanti.

Abdallah Kibaden aliwahi kuwa kocha wa Simba, Kagera Sugar na Ashanti.
Kocha wa zamani wa klabu ya Simba Abdalla ‘King’ Kibaden amefariki dunia leo.
Kibaden ambaye alichaguliwa kuwa kocha wa Simba mwaka 2013, pia aliwahi kuwa kocha wa Kagera Sugar na Ashanti United.
Baada ya Sunderland kufungwa 5-0 na Yanga 1968 iliamua kubadilisha kikosi chake kwa kuwaondoa wachezaji wakongwe na kusajili wachezaji chipukizi.
Miongoni mwa chipukizi hao walikuwa Abdallah Kibaden, Willy Mwaijibe, Omary Gumbo,nk. mwaka huo Abdallah Kibaden alichaguliwa katika timu ya taifa ya Tanzania na vile vile  alikuwa mwanasoka bora wa Tanzania.
Mchezaji huyo ambaye ana elimu ya ufundi magari Daraja la Pili (Motor Vehicle Mechanics Grade II) amewahi kuajiriwa katika kampuni mbalimbali, ajira ambazo kupatikana kwake kulichangiwa na kipaji chake cha soka.
Wasifu wa Kibaden
Oktoba 11, 1949: Alizaliwa Kiburugwa, Mbagala jijini Dar es Salaam.
1959: Alitungiwa jina ‘Kibaden’ na watoto wenzake kwa kucheza soka ya nguvu akiwa mdogo na mfupi. Jina lake halisi ni Abdallah Athuman Seif. Kibaden maana yake ni kitu cha baadae.
1969: Alijiunga na Simba FC, iliyokuwa ikiitwa Sunderland.
2011: Alikwenda Hijja.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Taarifa zaidi kuhusu kifo chake zinakuja…

No comments:

Post a Comment